Naombeni msaada wa kisheria wadau

Bomandamo

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2014
Posts
651
Reaction score
386
Nina duka langu dogo tu maeneo ya Sakina Arusha la spare za pikipiki, ndio nimefungua juzi, sasa leo TRA wanapita mitaani wanadai leseni, mimi sikuepo nilikua nimetoka, sikufunga duka ila kuna grill ipo kwa ndani nilirudishia na na kuweka kofuli ila unaweza tu ukaona vitu vilivyowekwa ndani.. sasa nimerudi nimekuta TRA wamefunga kabisa mlango na kuweka kofuli yao na kofuli yenyewe ni ndogo...

Sasa wasi wasi wangu ni kwamba huku hua wanavunja na kuiba vitu vilivyomo ndani kama hakuna mtu anaelala hivyo huwa mtu lazima alale ndani,

Wasi wasi wangu ni kwamba, je ikitokea leo usiku watu wakaja kuvunja duka wakaiba vitu kwa maana hakuna mtu anaelala ndani naweza kuwashitaki na kurudishiwa vitu vyangu?

Sasa kilichopo mimi naacha alafu kesho asubuhi nikikuta pamevunjwa nawahi polisi kutoa taarifa kwamba TRA wamefunga duka langu na nalalaga ndani hivyo sikuweza na matokeo yake nimevunjiwa na kuibiwa vitu, sasa je naweza nikawashitaki TRA na kulipwa vitu vyangu? Naombeni msaada kwa hapo wakuu ili kama kuna uwezekano nisipate kitu nikakae hapo nje kama mlinzi mpaka asubuhi kesho nikafuatilie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…