Naombeni msaada wa kisheria

monde arabe

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2017
Posts
8,781
Reaction score
13,444
Habar wanabodi,
husikeni na mada tajwa hapo juu.Moja kwa moja kwenye mada

Kuna shamba/kiwanja ambacho Mama yangu mzazi alianza kukimiliki kuanzia mwaka 1972 (During an era of villagelization).Watoto wake sote tumezaliwa na kukulia kwenye shamba/kiwanja hicho yangu alipokabidhiwa na serikali kama mmiliki halali

Mnamo mwaka 1999,nikiwa mdogo sana na sikuwa na ufaham wa kutosha tulihama kwenye eneo hilo na kwenda kuishi kwingine (mama na sisi wanae),ndani ya mwaka huo huo (yaani1999) kuna mtu alienda kupanda mahindi ktk shamba hilo bila kumuomba au kuzungumza na mama yangu mzazi ambaye ndiye mmiliki halali wa shamba hilo

Kilichofuatia,mama na huyo Bwana walipelekana kwenye vyombo vya sharia (baraza la ardhi) na huyo Bwana alishindwa kesi lakn kwa bahati mbaya mama yangu mzazi hakuweza kupewa nakala ya hukumu

Mwaka huo huo (1999 mwishoni) tulirudi kuishi kwenye kiwanja hicho
Mwaka 2016,mama yangu mzazi aliondoka kwenye kiwanja hicho baada ya sisi wanaye kumjengea nyumba sehem nyingine

Mwaka huu 2017,yule Bwana aliyeshindwa kesi mwaka 1999 amekuja tena na kumwambia mama kuwa amkatie japo nusu ya shamba na yeye ajenge na asipofanya hivyo atamnyang'anya shamba lote

WASIWASI WANGU;ni kwamba huyu Bwana anayo maeneo makubwa sana jirani na hapo kilipo kiwanja cha mama yangu mzazi,huwa anayalima na huwa hayamalizi kwa kuwa ni makubwa na ni mengi;ikitokea amepewa eneo na mama yangu mzazi,baadae ataanza kusogeza mpaka ( kwa sababu mikatani ndyo inayotumika kutenganishia mipaka) pia,kwa kuwa huyu m2 ni mlevi atakuwa anamtukana mama yangu mzazi matusi ya nguoni mpaka baadae ataamua kuliacha au kumuachia shamba hilo kwa kuwa huyu Bwana huwa anadai hilo shamba lilishawahi kuwa la kwake b4 villagelization period (villagelization ilianza 1972)

Pia,mama yangu mzazi walishatengana na Mzee muda mrefu sana so,hana m2 wa kuweza kumsaidia hata kimawazo,vilevile wakati mama yangu mzazi wanaoana na Baba yangu mzazi Tayar mama alikuwa ni mmiliki halali wa eneo hilo kwa muda mref sana
Tafadhalini naombeni msaada wenu wa kimawazo enyi wajuzi wa sheria
Asanteni sana!
 
Kiwanja hicho yangu alipokabidhiwa na serikali=kiwanja hicho mama yangu alipokabidhiwa na serikali
 
Msimpe

Akitukana mwekeni ndani

Matusi na tresspass

Na mkiwawezesha mbona mwaka mpya atauonea ndani

Akitoka ana adabu

Ila solution mjikusanye mjenge ukuta au nyumba
 
Msimpe

Akitukana mwekeni ndani

Matusi na tresspass

Na mkiwawezesha mbona mwaka mpya atauonea ndani

Akitoka ana adabu

Ila solution mjikusanye mjenge ukuta au nyumba
Asante sana Mkuu kwa ushaur wako,nataka January nikaweke bicon kwenye hicho kiwanja!
 
Mkuu hapo hakuna kesi, labda huyo jamaa mshikeni Mmpeleke polisi kwa tresspass na makosa mengine kama aliwai kutishia kuua na matusi ya nguoni.

Mbele ya macho ya sheria eneo ilo ni lenu kwa asilimia 99, kuanzia muda mliokaa, muda mliotumia kupaendeleza hapo haya mawili tu yanawapa uhalali wa kulimiliki eneo ilo mtakavyo, coz sheria inamtazama mtu alieiendeleza ardhi husika kwa miaka 12 kua nae ni mmiliki halali wa ardhi hio, sasa hapo bado hatujaongelea maswala ya sera za ardhi, maswala ya kesi mliyowai kushinda nk. Msipoteze muda mkamateni huyo mlevi.
 
Nashukur sana kwa ushauri wa wenye thamani kubwa Mkuu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…