Naombeni msaada wa kisheria

MadamG

Senior Member
Joined
Feb 1, 2013
Posts
125
Reaction score
47
Nilinunua shamba mwaka 2014 tuliandikishana ofisi ya kijiji mbele ya mtendaji na Mwenyekiti was kijiji Mwanambaya mkuranga ila mwaka huu naambiwa shamba sio langu na yule alieniuzia kwenda ofisi ya kijiji nakutana na Mwenyekiti akatukutanisha na muhusika Ila akaniambia aniandikie karatasi nisaini nikubali kubadilishiwa eneo nikakataa kusain kabla sijaona eneo nikaomba kuonana na mtendaji bahati nzuri mtendajiniliemkuta no mwingine siyo yule aliekuwepo kipindi mile akamwambia muhusika I'll eneo amwonyeahe yeye kwanza aridhike kuwa Galina tatizo ndipo ataniita kuandikishana ila yule muhusika hakuonekana tena nilipowasiliana nae akaniambia tukutane ofisi ya kijiji vikindu nikamuhuuliza inakuaje akaniambia huko anaenda kuniandikishia atanipa eneo language link mi nikaenda ila ilibidi nimkamate kwakuwa nilishaona dalili za kutapeliwa pale ofisi ya vikindu nilimkuta mtendaji was kipindi tuna and I Kishinev hati ya kwanza. Baada ya kumpeleka police ndio nagundua hats majina waliyotumia kwenye ile hati sio yao halisi muhuzaji pamoja na shaidi take ambaye ndie mjumbe alieniaminisha shamba in LA mtuhumiwa! Mwenyekiti na mtendaji waliitwa police wamekubali kuandika ile hati ila sijajua wamejitetea vipi? Mpelelezi was kesi Yangu aliniambia kesi ameshaipeleka mahakamani na imeshasomwa tar 9 mi sikuudhuria namuhuliza tar nyingine ya kesi akaniambia atafatilia aniambie ingawaje Mimi sins ulazima was kwenda mpaka Sikh ya ushaidi kwasababu kesi IPO mahakama ya wilaya, apo ndipo nachanganyikiwa hivi in kweli? He ntapata haki Yangu kweli na je naitaji niwashtaki mtendaji na Mwenyekiti kwa kunipa hati feki nafanya process zipi lengo language nipate haki Yangu tu.
 
Edit lugha ili waje wasome vizuri sasa na kukupa ushauri wale wataalamu wa sheria.
 
Madam haki yako utaipata lakini usiwe mvivu kufuatilia ,karibu kwetu kisemvule[emoji125]
 
Je katika hayo mauziano na ww ulikuwa na shahidi wako aloshuhudia mkiingia hayo makubaliano ?????

Ilikuwaje hao wawili hapo chini hawakuambatanishwa katika hilo shauri ???

Fuatilia kwa ukaribu sana shauri lako usije ipoteza haki yako,
 
Hapa angekuwa mkubwa wa kazi lissu kazi imeisha zaman

Lissu lud bhana tumekumiss
 
Caveat emptor =buyer be ware.

Kabla ya kununua ardhi (hata kama ni kiwanja kina hati) inabidi ufanye "land search" ambapo utaenda wizara/idara ya ardhi utalipia fee utaangaliziwa usalama/uhalali wa muuzaji wa eneo unalotaka kununua.

Hapo haki unayo ila kuna kitu ulifanya kinaitwa "contributory negligence" yan uzembe wako ulichangia wewe uibiwe. Haki utapata, ila kazi unayo.
 
Je katika hayo mauziano na ww ulikuwa na shahidi wako aloshuhudia mkiingia hayo makubaliano ?????

Ilikuwaje hao wawili hawakuambatanishwa katika hilo shauri ???

Fuatilia kwa ukaribu sana shauri lako usije ipoteza haki yako,
Shahidi anashuhudia mauziano. Unamuunganishaje kwenye shauri?? Yeye anabaki shahidi tu wa mauziano, suala la kwamba mali mnayouziana ina mgogoro au la ni suala la muuzaji na mnunuzi.
 
Shahidi anashuhudia mauziano. Unamuunganishaje kwenye shauri?? Yeye anabaki shahidi tu wa mauziano, suala la kwamba mali mnayouziana ina mgogoro au la ni suala la muuzaji na mnunuzi.
Msomi hujanielewa , Sikumaanisha shahidi kuhusishwa katika shauri,niliulizia suala hilo ktk kuuongezea nguvu mkataba huo wa kilaghai ulofanyika ya kwamba ni kweli umefanyika...

Mimi niloulizia hawakuambatanishwa kama washtakiwa ni hao wawili chini ktk maelezo yake ambao wameshirikiana na hao wengine katika kufanikisha hilo
 
Ni kweli andika vizuri ili usomeke vinginevyo watu hawaelewi unachosema mkuu na itakuwa vigumu kutoa ushauri kwa mada isiyoeleweka vizuri mkuu!
 
Je katika hayo mauziano na ww ulikuwa na shahidi wako aloshuhudia mkiingia hayo makubaliano ?????

Ilikuwaje hao wawili hapo chini hawakuambatanishwa katika hilo shauri ???

Fuatilia kwa ukaribu sana shauri lako usije ipoteza haki yako,
Nilikuwa na shaidi ila mtendaji na Mwenyekiti hawajaingizwa kwenye kesi nilimuliza mpelelezi wa kesi Yangu police anasema anawatumia kama mashaidi wa upande watuhumiwa kwakuwa waliandika majina sio yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…