Kwa kutumia sheria ya madhara "Law of tort" unatakiwa ufungue shauri la madai mahakamani, lakini lazima uweze kuthibitisha madhara uliyoyapata kutokana na habari iliyotangazwa, pia uthibitishe kuwa mtoa habari husika alikuwa na lengo la kufanya udharaulike mbele ya jamii na kwamba habari hiyo haina ukweli wowote. waweza kukishitaki chombo cha habari pamoja na mwandishi/mtangazaji wa habari hiyo. Mahakama ikiridhika waweza kulipwa fidia kulingana na madhara uliyoyapata na umaarufu/heshima uliyonayo.
Hili laweza kuwa somo hata kwa sisi tuliomo humu jamvini tujiepushe na kashfa au uzushi kwani teknolojia ikitumika utajulikana hata kama umeficha ID yako.