Naombeni msaada wa mawazo

Naombeni msaada wa mawazo

mkalusanga

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2013
Posts
369
Reaction score
446
Heri ya Mwaka Mpya Wana JF Wote!

Ninaomba msaada wa mawazo kama kichwa cha habari kinavyosema. Kuna mtu amenipa wazo la kufungua kiwanda kidogo cha juice na kuwa washirika wa biashara (business partners). Tumejadili kuhusu kupakia juice vizuri, kuipa jina, na kuifanya iwe ya kuvutia.

Sasa, naomba kujua: mbali na watu wa mazingira kuja kukagua, ni hatua gani nyingine natakiwa kuchukua? Je, TRA na TBS wanahusika? Naomba maelezo kuhusu taratibu muhimu za kufuata ili kuanzisha kiwanda hicho.

Pia, nataka nijue kama biashara hii italipa kabla ya kuwekeza pesa zangu nilizosotea. Siwezi kuingia kichwa kichwa bila kufanya tathmini ya kina.

Ninajua humu JF kuna majibu ya uhakika na yaliyoenda shule. Hili jukwaa kwangu ni kama Google JF! Nasubiri mawazo na ushauri wa kujengana.

Asanteni sana!
 
Back
Top Bottom