Naombeni msaada wapendwa!!!!!


Respect babu yangu!!
God bless you!!
 
LD dada yangu yaani NIMEUMIA kweli yaani nimeisi kama vile ni mama yangu anafanyiwa hivyo hata hivyo huyo mama bado hajachelewa kuna vyuo vingi vya ujasilia mali au vitu vingi vya kina mama vya kujifunza mbinu mbalimbali za maisha anaweza kuungana nao halafu ule ujuzi atakao upata pale akautumia pia ktk maswala yake binafsi ila asikose sana furaha mwambie yote hayo ni maisha na badala yake haji wajibishe ataona maisha yana kwenda smothly mwambie namtakia kila la kheri ktk maisha mapya atakayo anza baada ya kumpatia ushauri
 
nashukuru sana LD kwa mchango wako yaani ulikuwa umetulia na yule dada ameisha mkubalia baba yake kuhuswala la ndoa ya mama wa kambo
 

Pole sana Bakarikazinja.
Na asante kwa maombi yako, Mungu akubariki na wewe,
Tuwaombee mama zetu maana nasikia kuta zingekuwa zinaongea, tusingekuwa tunakatisha mitaani.
 
Jamani wadada nimerudi nimekuta bado mnaongea. Yaani hayo mazungumzo yenu yana hisia experience zinasikitishaaaaaaaa.

But I have personally learned a lot from you ladies, respect kwa sana
 
mwanamke mwenye akili timau lazima awe na sifa hizi

awe na akili timamu
awe na mawazo chanya
awe anamchalleange mumewe
ajue kutnza familia
ampende mumewe


huyu ni mama wa ndani ni mjinga sana na hata kama ni mimi ningeoa mke mwingine tena bila kificho
 
nashukuru sana LD kwa mchango wako yaani ulikuwa umetulia na yule dada ameisha mkubalia baba yake kuhuswala la ndoa ya mama wa kambo

Tumshukuru Mungu kama Amani ipo, wakati mwingine siri ya haya maisha hapa duniani ipo mikononi mwa Mungu pekee!!
Tuwaombee amani, na Mungu ambariki huyo mama awe baraka katika hio familia.

Ubarikiwe sana!!
 

Thanks Edson, ila kuna swali moja naomba nikuulize,
Haiwezekani ukamsaidi huyo mke wa jinsi hiyo akafanafana na vile unavyotaka??
 
halafu katika hii taarifa yako hujaonyesha mahali amabapo huyu mama ananyanyasika maana alipewa biashara akaiua.....mumewe kajitahidi kumkeep bize lakini mama hajitambui...yeye ndo maana mzee akaamua kumwacha kae home, ale, avae, alee watoto, ampe unyumba nknk

mpango wa nje wa mzee umesababishwa na huyu mama,,,,,pengine hapo alipo hajui haya unayoandika humu wewe.....
 
Thanks Edson, ila kuna swali moja naomba nikuulize,
Haiwezekani ukamsaidi huyo mke wa jinsi hiyo akafanafana na vile unavyotaka??


kwa jinsi ulivyoeleza huyu mama ana tatizo kubwa juu ya backgraound yake...hasa familia aliyotoka...siku hizi kina mama wako bize unamkuta mama yuko bize na kukopa sakosi ili walau akjikeep bize...

sasa namna ya kumsaidia huyu mama ni kufanyya ''total metanoia'' kwenye akili na ndani kabisa ya nafsi yake ..sio swala la kuamka asubuhi na kumwambia badilika......kwa jinsi nilivyoelewa ni kuwa mumewe anampenda sana ila his choice didnt work out the way he thouth it would be...... ndo maana ameamua kumwacha akae hapo home na huyo mwingine (plan B) amsaidie mumewe kuendesha familia
 
Huyo baba kitu anachokifanya si kizuri, kwani numba ndogo haitakiwi kwa mujibu wa dini yake.

Pili kwa sababu yeye alijikuta ameshaoa mama wa nyumbani angejitahidi tu kukomaa naye pengine angebadirika tu, kwa sababu huyo baba hana jinsi kama aliyavulia nguo anatakiwa kuyaoga.

La mwisho ni kweli ukisoma sana ukaoa mke ambaye kuna gap kubwa la elimu kuna kazi kubwa sana kwanza kwa ujumla hata mambo mengine ukimwambia haelewi kabisa. Mie ni shahidi kuna jamaa yangu sasa ana masters haf mkewe std 7, kwa kweli mipangilio yote huyo baba ndo anafanya. Kuna wakati alijaribu kumfungulia biashara mkewe ikashindikana maana hata chenji hawezi rudisha ikawa ni hasara juu ya hasara.

Pia mwanamke anaweza akawa ameishia la 7 lakini kichwani zimo, pengine hakusoma kwa sababu za kiuchumi na mila na desturi za wazazi hasa k
abla ya kuwa na shule nyingi za sekondari za kata. Huyo ukimuelekeza anaelewa vizuri sana. Ila kuna wengine ni mizigo kabisa.
USHAURI
nawashauri kaka zangu wa jf ambao hamjaoa, jaribu kuoa mtu ambaye hamjatofautiana naye kelimu, walau awe amemaliza form six kama wewe una elimu ya degree na kuendelea. Kwa kweli hata wale ambao wameshaoa watu ambao kuna gap kubwa la elimu huwa wanajuta kwa kiasi kikubwa sana.
Yule mama aendelee kuvumilia na kumuomba Mungu, kuna siku isiyo na jina huyo baba atabadirika tu. Mungu anaweza.
 
dada yangu LD ngoja nikwambie kitu dada..... kulingana na hii habari yako huyo baba atakuwa amejitahid sana kumbadilisha mkewe tatizo lakini mama habadiliki..... hii moja

huyo baba alichooona ni kuwa kwa kuwa wakati wa uchumba hakuona dosari kama hii leo akiwa ndani ya ndoa ameamua kumwacha na huyo mama hapo ili awe uthibitisho kwa jamii kuwa baba flna ameoa mke wa ndoa flani... lakini jamaa hayupo kabisa na hii imechangiwa na mama mwenyewe maana mama habadiliki..... hii mbili

uzee wa huyo jamaa unaweza kuwa wa manung'uniko kwa chaguo alilo nalo...ndo maana ilio mambo yake yaende amepata mtu mwingeni wa kumshauri na katika kushauriana penzi limechipua......

kingine nikwambie dada ...mkiwa kanisani then padre/mchungaji akasema ninyi ni mwili mmoja... huo mwili mmoja huwa haupatikan siku ya kufunga ndoa dada huwan ni process ya mda mrefu na hii inatokana na mambo haya yafuatayo:

mawasiliano ndani ya nyumba
jinsi mnavyopanga mipango yenu ya maisha na familia
mambo yenu ya chumbani(malovedavi) mnavyofanya na usafi wa miili yenu
na mengine mengi

sasa hapo katikati kunaweza kutokea lolote na kama mmoja habadiliki na hataki kubadilika ule usemi eti ninyi ni mwili mmoja huwa unasepa
na mwisho matoke yake ni kama haya
 

Daaa ubarikiwe Edson,
Hapo kwenye red kuna kitu nimekipata.
 
Duh Edson taratibu bana........LD hajasema kama huyu mama mwenye nyumba hana sifa hizo ulizotaja hebu mspee kidogo pengine mazingira yanamnyima kuekisesaizi hayo yote
 

Thanks in adavance.
Nimejifunza kitu kikubwa sana!!
Ubarikiwe zaidi na zaidi.
 
1. Nafikiri huyo baba alioa kwa vigezo alivyoviangalia yeye na inawezekana suala la elimu halikuwa kigezo muhimu kwake.
Siwezi kusema amekosea au hajakosea.


2 kutokumuendeleza huyo mama ni kosa analofanya huyo baba. Ila wapo wanaume wengi wakishaoa na wanaona wana pesa huwa wanajisahau kuendeleza wake zao.
Bora huyo aliyeonesha moyo wa kumfungulia mkewe biashara.
Inawezekana pia huyo baba alishaijua akili ya mkewe mapema kwamba hata ikipelekwa shule haiwezi kuchangamka.
Pia inawezekana huyo mama hakuonesha uhitaji wa elimu.

3. Kwakweli ni vizuri kuoana watu ambao akili zenu zinaendana. Tena akili za maisha. Mungu asaidie.
4.simlaumu huyo baba kumfanya mpango wa kando mshauri.
Tena nampongeza kwa kuwa utilized vizuri na mpango wa kando otherwise familia yake ingeyumba.
Ila namlaumu kwa kuwa na mpango wa kando wakati ana mke na ninavyoona hakuna anachokosa kwa mkewe.

Mwisho: namwambia huyu mama kuwa yeye ndio ana mamlaka na mumewe na kila kitu kinachohusu familia.
Yeye ndio wa kujipa furaha. Wanaume wana power lakini sisi ndio tunaowapa hiyo power.
Mwanaume anafanya kile ambacho sisi (wanawake) tutaruhusu akifanye.
Mwamuzi ni yeye, kama anataka kuitokomeza hiyo hali anaweza na kama anataka kuzidi kuikumbatia pia anaweza.
 
kuna hii sentensi ipo chini ya habari yako ''hata house girl anaweza akamfokea!!

dada LD mi nakwambi huyo mama ana matatizo hayuko sawa kichwani....kabisa... some thing is missing somewhere in her mind...

''willy-nilly'.....tunarudi kwenye point yanbgu ya mwazo...chunguza familia aliyotoka sio bure dada yangu.... pia ili abadilike ''total metanoia'' ( total change) hasa kwenye brain na kwenye ''soma'' (body) inatakiwa vinginevyo basi tuseme kalogwa na kageuzwa njepndani ndo maana yuko vile

''
 
kuna watu huwa hawaelewi....unamkuta mtu anasema hivi '' watoto wangu nimewakuza na kuwalea kwa shida/raha''

kuna kitu huwa wanakosea siku zote mzazi hamkuzi mtoto ila mtoto ndo huwa anamkuza mzazi.......

ni hivi jinsi mtoto anavyokua wewe mzaz/mlezi akili ya kuhanagaika ili mtoto wako awe na maisha mazuri huwa inaongezeka... lazima ujue mtoto wako atavaa nini, atakula nini, akiugua nifanyeje (bima nk) ... kwa hiyo kama wazaz hawana akili na ufahamu namna ya kuwakuza watoto wao siku zoote familia ya aina hii huwa na shida sana.... kama mzaz mmoja hana ushirikiano na mwenzake basi watot nao watakuwa kwa shida sana... chukulia mfano familia hii( tunayojadili) baba nae angekuwa na akili kama za mama... yupo yupo tu.. hao watot wangekuwaje?....

kwa hiyo lazima mshikamane, mchukuliane, msaidiane, mpange mipango pamoja, matumizi na mgawanyo wa pesa uwe wazi ka kila mmoja...hakika familia itastawi sana na kuwa familia yenye kupigiwa mfano.....

siku zote mambo matatu yanayovunja ndoa za watu wengi ni haya:

1: mawasiliano
2: pesa
3: mapenz

nikianza kudadavua moja baada ya jingine seva za jf zinaajam....

utasikia watu wanasema '' ndoa za siku hizi hazidumu'' mi huwa nabaki nacheka tu mara utasikia'' ohh mabinti/vijana wa siku hizi ni shida tu'' ukweli ni kwamba kina dada wengi wa siku hizi huwa wanataka vitu vya papo kwa papo hawajali mda..... chukua mfano umeoa binti then unamwambia '' mke wangu tulime kwa miaka 5, na tufuge kuku hawa na baadae tuuze kisha tujenge nyumba na baadsa ya hapo tununue gari yaani mke wangu nataka tujiteske kwa miaka 10 tukiwekeza then baada ya hapo tutaanza kula mema ya nchi.... kina dada wa siku hizi anweza kukataa........ hii iko hata kwa kina kaka... mke anaweza kumoa mawazo mazuri then yeye ama kwa makusudi akadharau, au ndo alivyo anapiga tu matokea yake kila wanalojaribu kufanya linashindikana...............

ntaapload kijitabu changu hapa huenda kitasaidia
 

hii mada inanikumbusha mistari ya biblia;

A wife of noble character who can find? She is worth far more than rubies.
Proverbs 31:10

...Pamoja na mapungufu yake kielimu na uwezo wa kung'amua mambo ya kidunia, huyo mama mwenye nyumba amejaaliwa sifa zake kama mke mwema. Naamini ndizo sababu zilizomvutia huyo baba kumuoa.

Huyo 'kimada' anatakiwa ajielewe yeye ni business partner tu, NOT wife Material.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…