Naombeni msaada wapendwa!!!!!

Tukisema tujadili kwa misingi ya kikatoliki then baba kakosea sana.kwanza baada ya kumpata huyo mpango wa kando na kungonoana nae kwa 1st tym ilihitajika aende kwa padre na kuungama dhambi ya kuzini..pili kwa misingi ya ukristo ni imani kuwa ufalme ni wambinguni wala fedha na mali hazina thamani yoyotee..mwisho nauliza je? Kama ni mama ndio alikuwa msomi,kampa mumewe biashara ikamshinda,mama kapata dume la mbegu linaloelewa biashara na kuzaa nae picha ingelikuwaje? Mkuki kwa nguruwe eh?? Wacha niende facebook nikatizame inbox zangu nitarudi..nafunga kwa kusema..u can gain the whole world and lose ur life..mbarikiwe mpaka kuku wa jirani wahamie kwenu!!
 
Aisee nlikuwa sijaisoma thread vizuri:

Siku nyingine LD uwe unaandika maneno machache bana!

Will be right back
 

Muhosni wako ni ushauri mzuri sana huu ninakubaliana na wewe ila nina mashaka
1. Utakapowakutanisha na kuwaeleza ukweli juu ya mapato ya familia- Bimdogo anawezaanza kuleta dharau kuwa yeye ndo anayeendeleza familia na kumfanya bi mkubwa ajinyongee......
2. Hata bila kuletewa dharau, kitendo tun cha kumweleza Bi mkubwa kuwa - mafanikio yote yameletwa na huyu mwenzio ni sawa na kumwambia yeye ndoa hakuiweza.......

Nadhani Baba atafute ustaarabu wa kuinua confidence ya Bi Mkubwa hata kama ni kumpeleka kwenye vikozi vya Biashara.

N.B Hakuna ukomo wa elimu Muhosni kwa elimu yake ya darasa la saba am sure hawezikosa kikozi kitakachomsaidia ujuzi hata wa biashara ya kuunguza Batiki
 

1.Je huyu baba alikosea kumuoa mke ambaye hana kiwango cha elimu zaidi ya
elimu ya msingi??
Hakukosea hata kidogo. Mke mwema si lazima awe na kisomo kikubwa au awe mjasiria mali. Hata hivyo, mtu kukosa sifa hizo hakumfanyi awe mke mbaya. Ni lazima mama huyu atakuwa na sifa nyingine nzuri na ndio maana wamedumu kwa miaka mingi katika ndoa.
2.Je kwa nini huyu baba asimwendeleze huyu mama/mke wake kielimu
kidogo ili aweze kuchangamsha akili kidogo?
Kusoma ni zaidi ya kilimo, si kila mtu anaweza. Inategemea kama mke mwenyewe anapenda na anaweza kusoma.

3. Je ni vizuri mtu kuoa/kuolewa na mtu ambaye walau akili zenu zinaendena katika utendaji wa mambo hasa ukizingatia mipango na maono yako ya maisha?
Ni vizuri, lakini hiyo pekee haitoshi kuwafanya wanandoa muishi maisha ya furaha katika ndoa. Ndoa ya furaha inatoka kwa Mungu.
4. Je huyu baba anafanya makosa kumfanya mpango wake wa kando
mshauri wa mipango yake ya maendeleo zaidi ya mke wake?
Ni kosa kubwa sana. Ni muasherati tu. Kwa nini asimlipe kama consultant badala ya kuzini naye? Wanaume wengi huwa tunatumia kigezo hicho kuhalalisha maovu yetu. Mwanaume ni mjinga na elimu yake haimsaidii lolote.

Mwisho: Unamshauri nini huyu mama mwenye nyumba, ili aweze kuishi kwa furaha na amani katika ndoa yake?
Amwome Mungu. Na achukue tahadhari mme asije kumzolea ukimwi huko anakolandalanda majalalani. Nitamwombea Mungu amrudishe mmewe. Nakumba mtoa mada ukamwonye huyo unayemuita "MPANGO WA KANDO" aiche ndoa ya watu. Mwanamke hata kama ni purely wa nyumbani, ana baraka zake katika mafanikio ya mmewe.
 

unajua LD ni ngumu kujua walipokosea....manake mimi nina rafiki yangu alikuwa anafanya kazi kama housegal,akapendwa na kijana wa bosi wake,akampa mimba na later akamuoa......dada wa watu kaenda soma ushonaji.....nakuambia kwa mwezi anaingiza kipato si chini ya milioni 1.5,anapenda kazi yake na anakwenda.....ombi lake kwa mume wake la kwanza,niondoe kwenye utumwa wa kuwa tegemezi....mume akampa alichotaka......kukosa elimu haiwezi kufanya iwe ilikuwa kosa kuoana kwao......still nina amini huyu mama angesisitiza mumewe angemomesha......kuna ka uzembe kako kwa mama...

Ila sasa tujadili way-forward.....mama anapenda kujiendeleza? if yes, narudia,amuombe mumewe amuunge mkono....kukaa chini na kulalamika na kuumia hakumtatulii tatizo lake.......:hand:
 
Thanx Michelle haya mambo mamiangu yaache tu............... ni magumu
 
Aisee nlikuwa sijaisoma thread vizuri:

Siku nyingine LD uwe unaandika maneno machache bana!

Will be right back

Nimesikia babu, nilikuwa natamani niandike vyote nilivyoniona na kuvisikia,
hata hivo nimebakisha mengine mengiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!!
 
Msimamo wa babu ambao ndio hali halisi na ukweli ni huu:

Mwanaume hajawahi na wala hatakaa aridhishwe na mwanamke mmoja
Mwanaume hajaumbwa kwa ajili ya mwanamke mmoja.

Mama mwenye nyumba hana alichokosea....hata angekuwa na upeo sawa na mumwewe, ameenda shule kama mumewe, angekuwa mjasiriamali mzuri, mzuri kama Cleopatra....bado jamaa angetoka nje.....(mwanaume haridhiki kuwa na mwanamke mmoja, msisahau)

Baba kuwa na mpango wa nje pia hajakosea.....kwa kuwa hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke mmoja.

Alichokosea huyu bwana:
Kuzaa nje ya ndoa....kama mkewe hana shida ya uzazi kilichompeleka kutotoa huko nje ni nini?
Kumdharau mke wake.....Ameshindwa nini kufanya mpango wa nje kwa siri?
Kuuachia mpango wa nje kuendesha biashara zake....Likiingia limbwata hapo, au mzee akaRIP ghafla vilio vya watoto wake wa mpango wa ndani vitamlilia mpaka jehanamu atakapokuwa.

Huu ni msimamo wa babu na hauusiani na imani ya dini yoyote ya dini wala mashirika ya kutetea jinsia za watu!
 
Baba alikosea kuoa mtu ambae wamepishana sana kifikra kama alitaka zaidi ya mama wakuangalia nyumba na kulea watoto!!Pole kwa huyo mama kwasababu hata sauti atakua hana vile hata kuendesha kabiashara kake mwenyewe alishindwa!Na utu uzima wake kuanza kujifunza jinsi ya kumanage mambo ni ngumu kwahiyo ni rahisi kwa yeye kuvumilia na kukubali hali halisi kuliko kuondoka!
 
Naomba nitoe mtazamo wangu kuhusu hili swala, Huyu mzee kampenda sana huyu mama wa House ndo sababu waliooana na kuishi miaka hiyo!. Huyu mama wa house, tatizo sio kutosoma sana, huko kutulia na kutosheka ni maumbile yake. Hata angesoma sana, pia angekuwa na msimamo huo kimaisha. Kuna watu huwa wanatosheka na kushukuru, bila ya kutatarika maisha mbio mbio, kuchuma na miaka yaenda ukingoni haswa ukiangalia umri kama unavyo elezea.

Huyu Mzee, dini ndio inampinga, kama sio hivyo angeoa wote wawili, kwani michango yao yoote ni muhimu kwake!.
 
Ndo tatizo la wanawake kuwa wategemezi. Napinga hili jambo kwa nguvu zangu zote. Inabidi wanawake muanzishe mifuko ya kusaidia wa-mama kama hawa. Hapa kwangu ishu ni kwenye swali la nne. Ni kosa kubwa sana.
Inasikitisha kuona huyu mama ameshadumazwa kiakili. Na cha kusikitisha zaidi ni mwanamke mwenzake ndo anachangia hilo.
 

Duh Babu............ama kweli Mwacheni Babu aitwe Babu.............Ye wa kwanza kuliona jua bana.
 
LD naomba majibu ya haya maswali yangu tafazali:

Babu nahisi nimekujibu, kulikuwa hakuna makubaliano hayo kati yao kabisa babu.
Anajua na kinamtesa siku zote, ni neema ya Mungu tu imemshika huenda angekuwa amefika mapaya zaidi.
 

Asante babu yangu,
Lakini sasa babu, mbona akili yangu inakataa kuamini kwamba wanaume wote lazima watoke nje ya ndo?
Kwani wanaume hawafuati sheria na amri za Mungu?
 

Mi najibu maswali yako kama ifuatavyo
1: Kwa kizazi hiki cha dot.com kama hujao au kuolewa nadhani swali la kwanza linaaply, ila kwa hoa wazee wakati wao ilikua haina tatizo kabisa.

2: Kumuendeleza kielimu mtu inatakiwa na utashi wake kama anapenda au la....hivyo hatuwezi kumlaumu baba kwa kuto muendeleza mkewe. kama ulivyosema waote wapo more than 50's so hapa itakua ngumu sana kumuendeleza mkewe.

3: Kwenye hili kimaadili ni kosa, kwa sababu jamii yetu bado haikubali kuwepo kwa mpango wa nje ingawa hili jambo lipo. Tukija kwenye uhalisia, huyo baba afanyi makosa kwa sababu hata hizo faida zinazopatikana kutokana na bussiness wafanyazo zinawanufaisha wote.

4: Ushauri wangu kwa huyu mama, kwa sababu umri umeshaeenda awe na amani tu hata, awalee watoto wake na ahakishe wanapata mahitaji yote muhimu. yeye aendelee kumpenda tu mumewe na amueleze kua hata kama ana mpango wa kando heshima kati yake na yeye iendelee asiwe nadharau kwa familia yake.
 
Wakati wanafunga ndoa waliapa kuishi pamoja ktk shida na raha, iweje leo tuseme mke alikuwa hafai?? Kwani mwanaume alikuwa hajui kwamba mke wake ni std 7 ??

Hapa ni wazi tu kwamba jamaa kamchoka mke wake (yuko kwenye 50's) kaamua kutafuta vya nje. Ni muendelezo tu wa kusaliti ndoa. Ndoa sio elimu, mapenzi pia si elimu. Mnapo ungana kimaisha ni UPENDO PEKEE huwa silaha ya maisha yenu. Ndani ya UPENDO ndio kuna vitu kama mali, pesa n.k.

No excuses, jamaa kamchoka mke wake basi.
 
Asante babu yangu,
Lakini sasa babu, mbona akili yangu inakataa kuamini kwamba wanaume wote lazima watoke nje ya ndo?
Kwani wanaume hawafuati sheria na amri za Mungu?

Hao wanaozihubiri Amri za Mungu, hao mnaokwenda kwao kutubu dhambi zenu na kurudishwa sijui kundini......nawazungumzia hao hao.....ni waasherati na wazinzi wakubwa tena wazoefu!

LD kubali usikubali lakini ukweli ndio huu: Sisi waname haturidhishwi na wala hatukuumbwa kwa ajili ya mwanamke mmoja.... Na hilo si kwa binadamu tu; Angalia majogoo, mabeberu, simba, fisi, na wanyama kribia wote.

Kufuata Sheria Za Mungu huwa tunazifuata kinafiki!
 

Nakubaliana na wewe ingawa nilidhani kwamba bimkubwa umri umekwenda kidogo. pengine LD atufafanulie

Unajua kuna ile hali ya kina mama ku give up kwamba hawawezi tena kujiendeleza.

Lakini pia nadhani siyo kila mtu aliyesoma ni enterprising (myself included), kuna ambao hata hawajasoma na wanafanya biashara kubwa tu (ninao ndugu zangu wa hivyo)

Pia tuangalie pia kwamba huyu bimkubwa tunatarajia asome eti ili aweze ku engage mentally kama bimdogo. I think this is too ambitious and likely to disappoint bimkubwa zaidi kuliko hali ilivyo sasa.

So I thought the best way is to capitalize on the existing circumstances and capabilities

Nitashukuru tena kusikia what you think about my views
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…