Mkuu kama uko mbali na Dar (yaani uko mikoani), kwenye kufanya malipo ya kodi na ushuru mbali mbali usije ukarogwa ukamtumia mtu hela ya kulipa eti akulipie, haki ya nani utapigwa cha juu mpaka uchanganyikiwe. Wajinga huwa wanachakachua zile document za charges ili uone ushuru uko juu. Mimi niliwastukia maana walitaka kunipiga pamoja na kwamba dogo aliyekuwa anashughulikia alikuwa mtoto wa shemeji yangu. Dar hakuna watu!
Mara ya kwanza akaniambia kwa mdomo kabla gari halijafika sijui port charges, wharfage, shipping line, TBS inspection, C&F agency fee. Kote huko wanaongeza gharama sasa kama unajidai kuwaamini utawatumia pesa ujue umeumizwa. Sasa nilichofanya gari ilipofika nikaenda na mimi mwenyewe, dogo akanipeleka kwa hao dealers (X), wakajichanganya wakanipa mahesabu tofauti na aliyonitamkia kwa mdomo huyo dogo.
Alipoiangalia ile document waliyonipa yenye mchanganuo nikamsikia dogo anaweka msisitizo mbona imekuwa tofauti hivyo utakuwa umetoa sheet nyingine siyo ile, hapo hapo halmashauri ya kichwa ikacheza, nikajiongeza kwamba hapa nataka kupigwa!
Maana walitaka niwape hiyo hela walipe wenyewe eti mimi niende tu hotelini nisubiri gari itoke usiku. Nikaweka msisitizo hela yangu silipi kwa cash nitakuwa nalipa kwa control number kadri ninavyopata documents Bandari na TRA. Ha ha ha haaaaa wakalowa vibaya sana.
Mwisho wa siku nakuja kulinganisha mahesabu waliyonipa na document za serikali nakuta walikuwa wamenipiga 500k na usheeee! Shenzy kabisa!!