Joyce wohwoh
Member
- Sep 17, 2021
- 80
- 185
Hawajakutumia document yoyote?Naombeni msaada wazoefu wa kuagiza magari Japan.Nimeagiza gari japan limefikia hatua wamepakia kwenye meli na wamenijulisha jina la meli,tarehe ya kuondoka na kufika japo wamenambia huwa zinabadilika sometimes.sasa utata uko hapa sijatumiwa TRACKING NUMBER.ili niweze kufatilia meli iko wapi.wazoefu je ninatakiwa itumwe lini?
Real motor Japan.Umetumia kampuni gani
Yah bado sijatumiwa document yoyote,wameniambia watanitumia Bill of Landing through DHL.Hawajakutumia document yoyote?
Hata hawa pia wako vizuri Tu kwenye huduma zao.Real motor Japan.
Siyo landing mkuu, inaitwa Bill of Lading (BoL). Kwa vile wamekujulisha jina la meli na namba yake unaweza kuingia google ukaigugu hiyo meli. Utaona kwenye ramani kila kituo inapofika!Yah bado sijatumiwa document yoyote,wameniambia watanitumia Bill of Landing through DHL.
Binafsi nilipata documents well before gari hazijaondoka hukoYah bado sijatumiwa document yoyote,wameniambia watanitumia Bill of Landing through DHL.
Daah asante sana kwa mawazo haya hawa watu wanatupiga sana hasa wa mikoani maana tuko mbali,shukrani mkuu.Mkuu kama uko mbali na Dar (yaani uko mikoani), kwenye kufanya malipo ya kodi na ushuru mbali mbali usije ukarogwa ukamtumia mtu hela ya kulipa eti akulipie, haki ya nani utapigwa cha juu mpaka uchanganyikiwe. Wajinga huwa wanachakachua zile document za charges ili uone ushuru uko juu. Mimi niliwastukia maana walitaka kunipiga pamoja na kwamba dogo aliyekuwa anashughulikia alikuwa mtoto wa shemeji yangu. Dar hakuna watu!
Mara ya kwanza akaniambia kwa mdomo kabla gari halijafika sijui port charges, wharfage, shipping line, TBS inspection, C&F agency fee. Kote huko wanaongeza gharama sasa kama unajidai kuwaamini utawatumia pesa ujue umeumizwa. Sasa nilichofanya gari ilipofika nikaenda na mimi mwenyewe, dogo akanipeleka kwa hao dealers (X), wakajichanganya wakanipa mahesabu tofauti na aliyonitamkia kwa mdomo huyo dogo.
Alipoiangalia ile document waliyonipa yenye mchanganuo nikamsikia dogo anaweka msisitizo mbona imekuwa tofauti hivyo utakuwa umetoa sheet nyingine siyo ile, hapo hapo halmashauri ya kichwa ikacheza, nikajiongeza kwamba hapa nataka kupigwa!
Maana walitaka niwape hiyo hela walipe wenyewe eti mimi niende tu hotelini nisubiri gari itoke usiku. Nikaweka msisitizo hela yangu silipi kwa cash nitakuwa nalipa kwa control number kadri ninavyopata documents Bandari na TRA. Ha ha ha haaaaa wakalowa vibaya sana.
Mwisho wa siku nakuja kulinganisha mahesabu waliyonipa na document za serikali nakuta walikuwa wamenipiga 500k na usheeee! Shenzy kabisa!!
Asante mkuu.Siyo landing mkuu, inaitwa Bill of Lading (BoL). Kwa vile wamekujulisha jina la meli na namba yake unaweza kuingia google ukaigugu hiyo meli. Utaona kwenye ramani kila kituo inapofika!
Ushauri wa hovyo huu! Wote walioagiza gari kutoka Japan watakuwa mashahidi kwa hili. Gari ya Yard iko juu kuliko ya kuagiza.Acha na hii mambo ya kuagiza gari nje. Nenda yard kuna maga mengi mazuri na ya viwango unavyotaka. Pili mpaka gari ikufikie gharama zitakuwa kubwa sana kuliko ungeenda kununua yard. Kama upo na cash kanunue live bila chebga unachagua kama mtumba.
Kati ya kampuni bora sana,Real motor Japan.