Pole Kaka Kiiza...wakati mwingine ni vigumu kidogo kutoa ushauri wa kitabibu kupitia forums, kwa sababu kuna maswali meengi ninayotamani kukuuliza na kupata majibu papo hapo ili niweze kukushauri vizuri lakini inashindikana. Kama mafuta ya taa yalifuata wakati tatizo la Nimonia lipo tayari, nachelea kusema kuwa tatizo hilo la kifua limesababushwa na hayo mafuta ya taa, japo inawezekana likawa limekuzwa.
Kama mgonjwa ni mama yako, na wewe ni kaka yangu tayari...nafikiri umri wa mama utakuwa mkubwa na hivyo nafikiri anahitaji uchunguzi toka kwa Dr aliyebobea kwa masuala ya vifua. Nakushauri uende Tumaini Hospital Upanga opposite makao makuu ya jeshi umuulizie Dr Mabula Mchembe. Nadhani akimuona mama atatoa ushauri wa kitaalamu zaidi.