nimefeli 4m4 mwaka jana nimepata divisio 4. Naombeni msaada nijiunge na coz gani ili nipate ajira nzuri.
Pole sana dogo, but nakata kukwambia kuwa kupata Division Four sio mwisho wa safari katika elimu, bado una uwezekano mkubwa wa kuendelea katika elimu kama utahitaji kufanya hivyo. kwa mfano kama umepata Division 4 na una pass 3 namaanisha D 3 unaweza kuanza kusoma basic certificate katika chuo cha St. John university kwa kuchukua certificate ya Business administration, chuo cha Utumishi wa Umma TPSC unaweza kusoma koz mbalimbali kama Record Management, Public and Local Administration na nyingine nyingi tembelea hapa
www.tpsc.go.tz utapata information zao nyingi tu.
Pia kama umepata D4 katika matokeo yako, unaweza kujiunga na chuo cha Mipango
www.irdp.ac.tz kusoma certificate ya Rural development Planning ambazo zitakusaidia kuendelea na elimu ya juu hadi Diploma. na pia kama kwenye matokeo yako una pass 5 nikimaanisha A,B,C,D 5 unaweza kujiunga kusoma Diploma katika chuo cha St. john
www.sjut.ac.tz ambayo itakusaidia kujiunga na degree baada ya kumaliza mafunzo yako.
Kimsingi kama ulipata pass 2 tu katika matokeo yako, ikimaanisha ulipata division 4 ya point 33 ndo unakuwa katika wakati mgumu na inakulazimu kurudia mtihani wako. But kama ulipata pass 4 au 3 una uhakika wa kusoma mpaka Diploma Level ukianzia Certificate course lakin sina uhakika kama unaweza kujiunga na Bachelor, lakini ukiwa na Pass 5 unaweza kuendelea mpaka bachelor level, tembelea
www.nacte.go.tz utapata maelezo zaidi.
Usipate shida dogo na usikate tamaa, bado una nafasi ya kusonga mbele, watu walio wengi wanashindwa kuelewa kuwa kupata division 4 sio kufeli kiasi cha kukata tamaa, ila ninachojua mie kufeli ni kupata division 4 ya point 33, hivyo unatakiwa kusema kuwa umepata division 4 ya point ngapi ili tuweze kukusaidia.