naombeni msaada

naombeni msaada

oldd vampire

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2011
Posts
253
Reaction score
52
mimi ni mwanamke wa miaka 24 sasa,ninatatizo la kutoa harufu ukeeni,kuna kipindi nilishika ujauzito nikaambiwa kua kutokana na hili tatizo mimba yaeza toka na kizazi,na kipindi nina mimba ndio harufu ilizidi mpaka nikawa siezi kaa na watu
nikapewa dawa flgyl nikaambiwa nimeze kumi na dox,cipro na candistat,hyo ilikua august 2012 na nikapona,sasa baada ya miez miwili ikarudi tena,nikapewa the same medication,nikapona,saiv imerudi tena,kuna mtu kaniambia kua ni STD's,sasa najiuliza km ndio hiyo mbona mpenz wangu hajapata?na STD's si hua mtu wajisikia kama homa na uchafu watoka mwingi wa njano?mimi sitokwi na huo uchafu wala homa sina
maybe mimi ndio sielewi labda,inamaana vaginal odour inasababishwa na STD's tuu?na lilinianza nilipo shika mimba
 
Nenda Hospitali Kuu ukaangaliwe vizuri na Wataalam zaidi watagunduwa ni nini chanzo cha wewe kutoa harufu kwenye sehemu zako za siri sio tu kupewa dawa pasipo kugunduwa ni kitu gani kinachosababisha wewe utoe harufu kwenye sehemu zako za siri.@oldd vampire
 
Pole sana. Nafikiria inakera kiasi gani.
Kama alivyoshauri dr, nenda kwa dr bingwa wa wanawake na umuelezee. Atakupima kila kitu pamoja na std ikihitajika. Usisahau kumuuliza kama na mwenza anahitaji matibabu.

Wakati huu angalia usafi wako.
1 hakikisha unajinyoa vizuri
2 acha kufanya douching (kujiswafi kwa kujiingiza kidole ama kutumia douching machine). Hairuhusiwi kabisa, ni exaggeration tu ya usafi wa mwanamke, i promise you!
3 vaa lightly. Chupi za cotton, nyeupe ndo nzuri zaidi (unaweza kununua panty liners ukatumia). Usijirundikie skintites etc.
4 epuka kutumia tampon (zile pedi za kutumbukiza). Chupi zifue na kuanika juani endapo haukaushi na mashine. Zihifadhi mahali penye hewa (badala ya kuziweka.kwenye droo ama.kabati ungeweza kutumia laundry basket ama open shelve.
5 epuka matumizi ya sabuni za kunukia sana. Hakikisha unajiswafi kwa kutumia light soap si zaidi ya mara mbili kwa siku. Nyakati zingine tumia maji peke yake bila sabuni.

Kila la kheri.
 
angalau sasa nafahamu matunzo yake, kumbe ni kazi hivyo.
 
pole sana dada, Ebu chukua ushauri wa Mhe Mzizimkavu haraka sana hapo juu, utafanikiwa tu, pole tena sana
 
kama unatoa harufu kali na hio hali haikuwa hivyo mwanzoni au naturally hutoi harufu means umeambukizwa std nenda na mwenzio hospitali mpimwe mtibiwe,usijiamini sana dada yangu kama unaishi na mtu kinyumba kuna chance ya wewe kuambukizwa.hawa waume zetu hujui walipokuwa....ila inawezekana pia ni infection tu ya kawaida imepona ila kwa vile mumeo hakutibiwa akakuambukiza tena,vyovyote vile iwe ni yeast infection ama ni STD nendeni wote mkatibiwe na msifanye sex mpaka wote muwe na uhakika mmepona.
 
Back
Top Bottom