Naombeni tiba ya kisaikolojia: Mwenzenu nikipanda ndege huwa nawaza hatari tupu

Pole,utazoea tu, ila safari za ndege kwenda America ya kusini ni shidaa tupu,kuna vimbuga vya kufa mtu.
 
Soma kitu wanaita "Flight phobia". Sio wewe tu mwenye hilo tatizo. Ni wengi linawasumbua.
 
Pole,utazoea tu, ila safari za ndege kwenda America ya kusini ni shidaa tupu,kuna vimbuga vya kufa mtu.
Mnawezaje kuvikabili ukiwa huko angani
 
Kuna kitu kinaitwa "airplane turbulence ni shida," hapa watu huwa wanajinyea wanazimia na wengine kutoa mkojo bila taarifa, wale walioenda Brazil kutokea Dubai watanielewa! Siwezi sahau kombe la dunia 2014 Brazil.Nilipotua home hata pasipoti sikumbuki niliiweka wapi. Ukisikia bahati nasibu sijui ukishinda sijui upelekwe wapi kataa chukua hela!
 
Kabisa yaani! Yanini kupata tabu yote hiyo
 
Tiba yako πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ hii hapa Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)
 
Mie hata lift tu napata tabu, yani huwa napanda basi tu napo hadi pawe parefu kama ni gorofa 5- napanda ngazi....
 
Kamuone psychiatrist doctor atakuhudumia na utapona.

Utatakiwa uzingatie therapy na follow up na akiona vyema ataku prescribes pia.
 
Hali hiyo yaweza kuwa na athari hasi kwenye maeneo mengine ya maisha yako mfano kwenye mahusiano, afya ya mwili wako n.k

Kamuone daktari na mchungaji au Shekhe mwenye Ufahamu wa mambo na pia jizoeze kusoma Maandiko Matakatifu, Fanya mazoezi ya mwili hayo ukifanya yote kil moja kwa umuhimu wake baadhi ya muda mfupi utashangaa utakuwa umepona inabaki historia!
 
Asante kwa ushauri mzuri
 
Mkuu wewe ni Mhaya?
 
Kwa andiko hili unaonekana unazungumzia route za ndani,mm niliwahi safiri na Turkish airlines Safari ndefu kutoka Cologne kwenda Melbourne Australia wewe acha tu hiyo route ina misukosuko mingi mno,hasa ya bahari
Uliwezaje kuimudu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…