Naombeni TIPS za kuvutia wateja kwenye fastfood delivery

milionea wa kesho

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2015
Posts
328
Reaction score
631
Nimefungua kamgahawa katikati ya mji. lengo langu ni kufanya free delivery ya chakula kwa watu wenye maduka na wakazi waliopo karibu na mji. Ni mbinu gani naweza kutumia kukuza soko?
 
Naomba kukushauri kwa dhana nzima ya biashara ya chakula bila kuangalia kama unahudumua wateja moja kwa moja au unawapelekea majumbani au makazini mwao.
1.Ladha (Taste). Kubali au kataa uchawi wa biashara ya chakula ni ladha. kama chakula chako kina ladha mdomoni basi hata kama una wateja kimara watakuja tu kufuata ladha ya chakula ambayo yameshaizowea. Usione watu wanatoka Ubungo wanakwenda kula tabata ukidhani kama hakuna migahawa ya biriani Tabata ila ni ladha ya biriani ndo wanaoifuata Tabata

2.Usafi. Hapa namaanisha usafi kwa ujumla kuanzia jiko unakopikia, vyombo unavyotumia kutayarishia na kupikia pamoja na usafi wa wafanyakazi. isiwe unapikia vyakula sehemu chafu kwa vile tu unafanya delivery kwani vinaweza vikawaletea madhara watumiaji na wasikuagize tena

3.Uaminifu. Uwe muaminifu katika biashara yako na mikakati ambayo unapanga isiwe inabadilika kil abaada ya muda, mathalani leo wali nyama 1,500.00 badala ya siku tatu ishapanda na wateja hawana taarifa yoyote juu ya kupanda kwa bei.

Naamini kuna wengine wataanzia nmba nne kwendea mbele
 
Simple sana hiyo kitu, angalia mapungufu ya jiran zako, usiweke tofauti kwenye bei ila Kama ni Wali nyama ongeza na kachumbali, fresh juice kwa kuongeza bei kiasi ya msosi mfano Kama ni buku tatu basi uza buku 3. 5 ukiongeza na fresh juice ya ml 350.

Njia nyingine wauzaji wawe type ya Miriam birian, shape na sura alafu wasiwe na kiburi wala maringo hapa wateja utawakamata tu.

Njia nyingine ya kuongeza wateja hatakama sio kwa kudelivery hakikisha msosi mtamu mchuzi mzito sio minyanya haijakaangwa vizuri, vitunguu vimekuwa mkaa nk...

Hakikisha ni msafi kuanza muonekano wako hadi chakula chako na makapu ya kupelekea msosi sio yanakuwa meusi, mchuzi umegandiana.

Njia nyingine pita kwa waganga wa kienyeji wakusaidie [emoji16][emoji16][emoji16]

Kila la kheri, za kuambiwa changanya na zako.
 
upande wa ladha sina shaka kabisa kwa sababu nimepata mpishi wa kimataifa anapika rojo la sotojo hatari. yaani unafeel kabisa ladha ya utamu.

kwa upande wa usafi wa dada wa kazi bado kuna walakini kidogo ila nitajitahidi. hata upande wa jiko la kupikia pia sio safi sanA ila nadhani halina shida. nashukuru sana kwa mchango wako
 
mm ni mwanaume na nimetarget nakua nAwapelekea wateja wa kike. najijua ni msafi sana na handsome kwa mbali ([emoji23][emoji23])



nina wafanyakazi wawili wa kike ila sio type ya mariam birian. sio wazuri kivile ila wanajitahidi usafi. natamani sana ningepata wahudumu wenye sura nzuri na shepu.

kwa waganga bado sijafikiria.
 
Vizuri, mshahara utawafanya wawe wazuri, uwe unawapa tips na ushauri wa hapa na pale wananunua mafuta mazuri wanang'aa, usafi ndio ukomalie Sasa uli kuwe njema jikoni....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…