Alkelokas
JF-Expert Member
- Dec 12, 2012
- 203
- 103
Habarini zenu wakuu, nina suala linanisumbua kati yangu na jirani angu kuhusu mipaka.
Ni hivi jirani yangu kapanda mti wa mparachichi hii ya kisasa jirani kabisa na mpaka takribani nusu mita toka mpaka ulipo, sasa umekua na matawi mengi yamekuwa shambani kwangu ambapo nimepanda migomba inashindwa kuwa na afya sababu inakosa mwanga na matawi ya mti yametanda migomba.
Ni muda sasa nilimwacha tu kwamba huenda atapunguza mana hata yeye anaona hali ilivyo cha ajabu kanogewa na hela za parachichi hana wazo la kutoa tena.
Leo kulikuwa na ndizi iliyoko mpakani imekomaa ambayo kimsingi ilikuwa upande wangu imesogea hadi mpakani akamtuma mtu akate, mke wangu alimwambia asikate mana siyo yake.
Yule jirani akaja juu kwamba zamu yake kula maana ya mara ya kwanza tulikata sisi, ndipo mwanamke akamjibu kuwa mbona yeye mparachichi wake matawi karibu yote yapo shambani kwetu na yanaharibu migomba husemi? Basi tugawane parachichi lakini ndizi wewe zinakuuma?
Yule jirani ghafla akamuita Balozi wa Nyumba Kumi ndipo nikapigiwa simu nifike mara moja kwa usuluhishiu. Tuliafikiana migomba iliyo mpakani ikatwe na ndzi iliyokuwa imekomaa ikamuuliwa apewe jirani yangu.
Nilipouliza vipi kuhusu matawi yaliyo shambani kwangu maana yamekuwa yakiniathiri nikaambiwa na Balozi ni suala la kumuomba apunguze kwa maana mti ulipandwa kabla sijanunua pale. Nilipouliza utaratibu wa umbali wa kupanda miti mipakani ukoje, wakasema ishu niliukuta kwahiyo ni ombi siyo lazma!
Naombeni ushauri kisheria limekaaje kabla sijafanya maamuzi mengine, maana nimeona nisije haribu, maana nimeona kama wamekula parcent yule Balozi na Mjumbe.