Habari zenu wanajamvi.
Bila kupoteza muda naomba mnisaidie kunifafanulia hili swali.
Hivi kwamfano imetokea labda mtu ame-fake kifo chake alaf ww ndo ukaonekana umemuua ukafungwa miaka kadhaa jela kwa kesi ya mauaji, baadae unatoka unakaa uraiani baada ya miezi kadhaa unakuja kumuona yule mtu uliyesingiziwa umemuua sasa wewe kwa hasira ukaamua kumuua kweli sasa Je, utashtakiwa tena? na utashtakiwa kwa kosa gani?
Kama ni kosa la mauaji ina maana utaonekana umemuua mtu mmoja mara mbili au inakuwaje?