Wakuu heshima kwenu.
Natumai nyote mmekua na week end nzuri kama yangu.
Wakuu nahitaji gata zile za plastick.Nimeambiwa ziko gata kutoka South Afrika,Uturuki,Malaysia,China na Tanzania.
Nimeambiwa nzuri ni za South lakini siku hizi haziletwi tena,nikashauriwa nichukue za China au za Malaysia sababu eti zina afadhali kuliko za Tanzania.
Nimeambiwa niwe makini sababu naweza kuuziwa za China nikaambiwa ni za Uturuki.
Ombi langu hapa,ni naombeni mniambie duka ninapoweza kwenda kupata gata nzuri bila kubabaishwa au kuuziwa kitu ambacho sicho.
Natanguliza shukrani zangu.
Waone Nabaki Afrika
Watumie email info@nabaki.com
Asante mkuu,ntajaribu labda watajibu,tatizo siwezi kwenda huko walipo ingeniwia rahisi kama ningeongea nao kwenye simu ibakie kumtuma tu mtu akanichukulie.Sijui wabongo tukoje,yaani unapiga simu inaita weee haipokelewi,au labda muda wao wa kazi umepita nisiwalaumu bure,maana saa hizi sidhani kama ni lunch time,labda.Nimeboreka kidogo.
Waone Nabaki Afrika
Pole kama ni landline inaweza kuwa out of order jaribu hizi
Jeff Kayton
MARKETING MANAGER
HEAD OFFICE: 2/1 Sam Nujoma Rd, Mikocheni Light Industrial Area, next to Coca-Cola Kwanza (Mwenge)
P.O Box 11747, Dar es Salaam, Tanzania
Tel: +255 (0)22 2775138 or 2700635, Mobile: +255(0)766765505, Fax: +255 (0) 22 2775139
Email: jeff@nabaki.com Web : www.nabaki.com
MAIN BRANCHES: New Bagamoyo Road: 022 2647756 - MASAKI-Chole/Slipway Rds: 022 2601992
Yeah hao ndo wenyewe. Wana gutter za high quality na bei zao (kwa gutter) hazina tofauti na za maduka yasiyoeleweka huko Kariakoo na kwingineko.
Madam queenkami jaribu namba hizi lazima utawapata wahusika.
0757142170, 0789241001 au 0653774513
Asante mkuu nimeshawapata kwa landline.
Karibu madam,
kama ndo unamalizia nyumba yako na hujaweka vitu vingi watembelee incase upo TZ waweza kupata vitu vingine vizuri na vyenye high quality kwao. Kwa mfano wana mixer (mabomba ya maji) nzuri kabisa kutoka Ujerumani na bei zao ni nzuri tu etc
Nashukuru,vitu vya ndani vyote tayari nilichukua pale CTM nyerere Road,niliambiwa nao ni wazuri natumai ni wazuri kweli.
Ubarikiwe mkuu,tuko pamoja.