Naombeni ushauri juu ya hili.

bwii

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2014
Posts
1,429
Reaction score
2,669
Kama kichwa cha topic kinavyosema, naombeni ushauri juu ya hili la kula kwa mtoto wangu mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi nane.
Amekua hapendi kula kabisa na tumemjaribu kwa kila chakula mbalimbali lakin bado amekuwa mgumu, tumemweka awe anakula na watoto wenzake, sisi na watu mbalimbali lakini wapi.
Tulichogundua ni kwamba anapenda mayai ya kanga na kuku wa kienyeji ya kuchemsha,ukiyakaanga nayo hali(ya kisasa huwa ana nusa na kutupa) labda chips kidogo anaweza kula, ukimchemshia viazi navyo hali.
Je, kula mayai mara kwa mara inaweza kumletea tatizo? Anaweza kula hata matano kwa siku.

Ushauri wenu tafadhali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…