Naombeni ushauri juu ya kuongezeka kwa tumbo

Naombeni ushauri juu ya kuongezeka kwa tumbo

peho

Member
Joined
Oct 9, 2013
Posts
75
Reaction score
23
Jamani ndugu zangu wana JF.mwenzenu tumbo langu linazidi kukua siku hadi siku.sio mimba bali ni mafuta.nifanye nini ili kuepuka hii hali.
 
lipia gym uwe una fanya mazoezi, af kama utaweza nunua ule mkanda wa kuzungusha tumboni una punguza sana, iko maduka yaliko usawa wa benjamn mkapa parking tower, hii ndo njia rahisi
 
sasa kumbe unajua sababu halafu unaomba msaada,si uache mafuta?
 
Fanya fyongo kazini ili ufukuzwe kazi, baada ya miezi kama mitatu rudi utupe majibu
 
punguza vyakula vya wanga , tumia zaidi mboga mboga na mtunda ..
 
Noah kilo mbili,ndizi 4 kila siku lazima uwe na kitambi.
 
chkua unga wa mdalasini kijiko kimoja cha chai na asali kijiko kimoja cha chai changanya na maji ya moto kunywa kikombe kimoja kila cku asubuh kabla ya kula chochete na usiku kabla ya kulala itakusaidie mi hufanya hvyo naona tokeo.
 
Jamani ndugu zangu wana jf.mwenzenu tumbo langu linazidi kukua siku hadi siku.sio mimba bali ni mafuta.nifanye nini ili kuepuka hii hali.

Fanya mazoezi ya kukimbia kuinama na kuinuka kwa haraka haraka kila siku.Au kaa sakafuni inamisha kichwa mpaka miguuni harakaraka.Isipungue dak 60.Kwa ujumla ni mazoezi soma vitabu vya mazoezi ukizingatia wiki tatu utaona mafaniki😵nyo usisikilize maumivu ukajihurumia kwani hutafaulu.
 
Nitajie vyakula na vinywaji vyote ulivyokula na kunywa siku 3 zilizopita. NB: Kuwa mkweli lasivyo hatutapata ufumbuzi na kama hukumbuki basi anza kuandika leo na baada ya siku 3 zijazo niambie na nitakupa jibu. Usisahau kuniambia ni kazi gani unafanya.
 
Ndugu lyopoko siku 3 zilizopita kulikuwa na sherehe.kwa kweli sio siri nilikunywa bia kama crate moja hivi.ila wanga sijala.
 
Ndugu lyopoko siku 3 zilizopita kulikuwa na sherehe.kwa kweli sio siri nilikunywa bia kama crate moja hivi.ila wanga sijala.

loh creti zima! kwa vile ilikuwa bure kweli dezo inaua,unasema hujala wanga? hujui kwamba bia ni wanga? achana na bia kabisaaaa.
 
Back
Top Bottom