Kwa Outlander, asilimia kubwa vitu vinaendana na RVR ila maelezo zaidi ni kama ifuatavyo;
Mitsubishi Outlander ni Mid-Size SUV ambayo ina configuration za 5-seater na 7-seater. (Kuna ile ya kawaida, Roadest, PHEV (Plug-In Hybrid Electric Vehicle), so far kuna generation nyingi).
Gari hii ni kaka wa RVR ambazo Specifications zake zinafanana sana ukiachilia mbali ukubwa wa body, engine na sitting arrangement.
TRIM-LEVEL (DARAJA)
Gari hii inakuja na madaraja-2 yaani “M” Kama Basic model na “G” kama level ya juu kwa maana kwamba iko na features nyingi na ni gharama kidogo.
DRIVE TRAIN
Hapa kwenye kila Trim-level utapata chaguo la either 2WD au 4WD (Electronically controlled) kutokana na uhitaji wako
ENGINE (4B11 (CC2000), 4B12 (CC2400) & 6B31 (CC3000-V6))
2.0-liter (4B11), 2.4-liter (4B12) 16-valve four-cylinder DOHC MIVEC (Mitsubishi Innovative Valve-timing Electronic Control). Hapa nyingi zinazokuja Tanzania ni za soko la Japan, hizi zenye CC3000 ni soko la Ulaya ambazo kuna manual (Petrol na Diesel) v6 powered.
TRANSMISSION (Outlander ambazo ni common kwa Tanzania ni cc2000 na 2400)
INVECS-III (Intelligent and Innovative Vehicle Electronic Control System) 6-speed sport mode CVT (Continuous Variable Transmission)
SUSPENSION SYSTEM
Outlander employs a MacPherson strut front and a trailing arm-type multi-link arrangement rear suspension. The wider track and longer stroke improve handling and stability.
FEATURES
Gari hii inakuja na Paddle Shifters kama sport mode, Adaptive Cruise Control (ACC), Active Stability Control (ASC), Rear seat center armrest, HID headlight, Panorama glass roof (with LED illumination), Push-button engine switch for smooth engine start-up, Tilt and telescoping steering wheel to adjust the steering wheel height and angle for the optimal driving position na pia ina option ya DC (inakuwezesha kuchaji vitu kama Laptop, Camera, Simu) etc. hivi ni baadhi ya vitu vinavyopatikana kwenye Mitsubishi Outlander na kuvipata vyote kwenye gari inategemea na Trim-level ya gari yako.
ENTERTAINMENT
Outlander nyingi zina kuja BUILT-IN SUBWOOFER, ambayo ni Rockford Fosgate Premium Sound System for enjoyment of dynamic concert-hall quality sound. Pia ipo na COOLER BOX inayokupa nafasi ya kupoza vinywaji vyako vichache.
FUEL CONSUMPTION FIGURE
Angalia kwenye attachment chini.
CHANGAMOTO
- Gari hizi zina changamoto yaku-overheat gearbox kama ukiweka vilainishi ambavyo ni tofauti na manufacturer recommendation (Gearbox oil yake ni CVTF-J1 au J4, soma Dipstick yako), pia sababu nyingine ya overheating ni aggressing driving/rough driving maana CVT vehicle zina tumia gear ratio na ni smooth hivyo inachanganya yenyewe. Kingine kutobadilisha oil na filters za gearbox kwa wakati
- Hizi gari ni slow at initial acceleration ila ikichanganya ni moto wa kuotea mbali
- Gearbox belt sleep inayochangiwa na tabia ya mwenye gari kwa mfano wakati una reverse na gari bado inarudi nyuma ghafra unaweka Drive hii haitakiwi kwenye gari za CVT.
- Spare parts kidogo ni gharama japo zinapatikana na ukifunga zinakaa muda mrefu (Kuna options zote Mchina, Mjapan au toka Thailand)
Kwa ujumla Outlander ni gari nzuri, very comfortable, fuel economy nzuri and reliable kama utazingatia mambo yote ya msingi.