Naombeni ushauri katika wazo la biashara hii

GANG MO

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2016
Posts
2,092
Reaction score
2,210
Mimi ni kijana ambaye nilihitimu chuo mwaka 2016. Sikubahatika kupata kazi ya fani niliyosomea. Niliamua kuingia mtaani hapa mafinga na kupiga kazi za mtaani kwa bidii na nikawa naweka pesa benk. Sasa nimefikisha milion 10.

Wazo langu ni kununua bajaji na kuiendesha mwenyewe. Naombeni kueleweshwa katika mambo yafuatayo

[emoji117] bei ya bajaji mpya ni sh ngapi?.

[emoji117]baada ya kununua bajaji kuna hatua gani natakiwa kuzifuata katika usajili mpaka nafikia hatua ya kuruhusiwa kuanza kupakia abiria?

[emoji117]je ni changamoto zipi hujitokeza katika bajaji ambayo huendeshwa na mmiliki?

Ninawasilisha wadau.
 
mkuu bei ya bajaji ni kati ya m7 hada nane

Kuhusu vibali vya kufanyia kazi fika mahali wanapo paki bajaji na kuuliza utalatibu wao hapo utapata miongozo yote
 
Kuna uzi humu wa jamaa kuuza bajaji yake mpya kabisa ya Tvs kwa bei ya milioni 6 tu! tena ni bei ya kuanzia. Utafute huo uzi ili ukaichukue ile mashine. Mambo ya vibali na uendeshaji wake utajua tu mwenyewe utakapoingia kazini.
 
Ahsante mkuu ngoja nitafute
Kuna uzi humu wa jamaa kuuza bajaji yake mpya kabisa ya Tvs kwa bei ya milioni 6 tu! tena ni bei ya kuanzia. Utafute huo uzi ili ukaichukue ile mashine. Mambo ya vibali na uendeshaji wake utajua tu mwenyewe utakapoingia kazini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…