Naombeni ushauri kipi kifuate katika nyumba yangu, kama inavyoonekana pichani

Naombeni ushauri kipi kifuate katika nyumba yangu, kama inavyoonekana pichani

GREAT INVESTOR

Senior Member
Joined
Nov 13, 2018
Posts
128
Reaction score
297
Wadau, Wana Jf Kheri ya Christmas kwenu.

Wadau, pichani chini ni nyumba yangu niliyoanza kuijenga mwezi wa Sita inaenda kwa kusuasua ila namshukuru Mungu.

Nimekuja kwenu kuomba ushauri wenu, Nyumba yangu ina ukubwa japo si sana ila kwa uwezo wangu nasema ni kubwa, ina room 3 za kulala moja master, ina Choo cha public,jiko,sebule na store.

Uchumi si mzuri sana ndiyo sababu ya kuomba ushauri wenu.

Nimeshaifanyia plumbing, kuweka bomba kwa ajili ya waya za umeme na box kwa ajili ya socket na switches, pia nimeshaipiga draft kwa ajili ya gypsum,nimeweka grill pia.

Juzi nmeanza kuipiga plasta na sasa mafundi wanaendela.

Ila kwa sasa uchumi si mzuri sana,kwa maana ya kwamba nikiangalia mfukoni nina pesa si nyingi...ambayo inaweza kunisaidia kufanya moja Kati ya haya hapa chini.

1.Nifunge gypsum
2.Niweke alminium
3.Niweke tails.

Nimeipiga plasta japo sijaweka frem za milango ya mbao.

Kwa mwenye ushauri mzuri nifanye nini Kati ya ivyo apo juu kwa sasa, naomba unisaidie.

Pia naomba kuuliza je nimekosea kupiga plasta bila kuweka frame za milango?

Natanguliza shukrani.

IMG-20211223-WA0050.jpg
 
Weka tiles kwanza baada ya hapo piga jipsum bord au vice versa. Almunium fanya iwe kitu cha mwisho kabisa
 
Kwenye ujenzi hizo tiles ni kitu cha mwisho. Funga gypsum board ili skimming ifanyike pamoja, Kisha njoo na aluminium, ukimaliza aluminium njoo na rangi, ifuate tiles game over
 
Weka Aluminium kwanza ili paweze kufaa kuishi ikiwa utataka kuingia kuishi, kisha njoo kwenye gypsum na mwisho ndio tiles.

Sababu za msingi ni hizi.
-Unaweza ukaamua kuingia kuishi hata kabla ya finishing yote kukamilika ikiwa pako salama (kiafya na kiuhalifu) kama kuna Aluminium tayari.

-Gypsum inapaswa kuanza kabla ya Tiles ili kuepusha kuharibu tiles ikiwa zipo. Uwekaji wa gypsum hutumia ngazi, nyundo, rangi nk.

-Kwa nyumba kubwa, na ikiwa uchumi uko pagumu, suala la kuweka Gypsum au Tile linaweza kufanyika kwa awamu, kidogo kidogo, chumba kwa chumba
 
Kwenye ujenzi hizo tiles ni kitu cha mwisho. Funga gypsum board ili skimming ifanyike pamoja, Kisha njoo na aluminium, ukimaliza aluminium njoo na rangi, ifuate tiles game over
Shukran san kiongozi
 
Weka Aluminium kwanza ili paweze kufaa kuishi ikiwa utataka kuingia kuishi, kisha njoo kwenye gypsum na mwisho ndio tiles.

Sababu za msingi ni hizi.
-Unaweza ukaamua kuingia kuishi hata kabla ya finishing yote kukamilika ikiwa pako salama (kiafya na kiuhalifu) kama kuna Aluminium tayari.

-Gypsum inapaswa kuanza kabla ya Tiles ili kuepusha kuharibu tiles ikiwa zipo. Uwekaji wa gypsum hutumia ngazi, nyundo, rangi nk.

-Kwa nyumba kubwa, na ikiwa uchumi uko pagumu, suala la kuweka Gypsum au Tile linaweza kufanyika kwa awamu, kidogo kidogo, chumba kwa chumba
Shukran sana
 
Back
Top Bottom