Naombeni ushauri kuhusu hizi undergraduate degree programmes

namanyele

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2012
Posts
1,852
Reaction score
610
Heshima kwenu wana jf,naomba wenye kufahamu kuhusu hizi programmes mbili wanisaidie kunielewesha vizuri

1.Bachelor of Community Economic Development(BC EDP)

2.Bachelor of Arts in Economic(BA ECON)


*sasa ni ipi ambayo iko hot zaidi katika soko la ajira kwa sasa? ni hilo tu wadau
 
BA Economics iko poa sana,hyo nyingne utapoteza muda wako bure 2.
 
Unaposoma usiangalie soko la leo. Hadi unamaliza soko litakuwa limeshajazwa.Utakuwa kama mnajeria mwenye degree nyingi kwa sababu kila moja aliisoma baada ya kuambiwa tunahitaji mtu wa fani husika, akirudi imejazwa, naendea nyingine akirudi imejazwa....Soma ukiangalia miaka 10 hadi 20 ijayo.

Pia penda kusoma degree ambayo ama nifani mpya kabisa ama inatoa mwanga wa kuweza kujiajili na sio kuwaza kuajiliwa tu. Mwisho, usichague degree fulani eti kwa kuwa kuna mtu alisoma hiyo degree na sasa ana maisha safi. Utakuwa umepotea.
 
Mkuu eedoh05 nashukuru kwa ushauri wako hapo juu,umenifumbua macho kiukweli mana kuna watu wenye degree zao ambazo zilionekana market enzi zile leo hii hawana kazi,nilikata sana tamaa ya kusoma lakin kwa huo ushauri ngoja nitulie niufanyie kazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…