Kuhusu idadi, itategemea ukubwa wa eneo lako, ukubwa wa mtaji wako na utayari wa banda.
Mimi binafsi nina style tofauti ya kuanza mradi kama huo.
Lengo langu nifikishe kuku 2000, lakini nilianza na kuku 50, na kila mwezi ninaongeza vifaranga 100, kwa hiyo baada ya miezi 6 nitakuwa na kuku 650, Malengo, wakishaanza kutaga, mayai 300 ya kwanza natotolesha kwa incubator round ya kwanza, wakitotolewa naweka round ya pili tena mayai 300, na kuendelea. Hapo mradi utakuwa unajiendesha wenyewe mpaka wafikie idadi unayotaka