Naombeni ushauri kwa hili..

Joined
Jun 30, 2013
Posts
21
Reaction score
14
Asalaam wana JF,

Nimekuja hapa ili nipate ushauri ama nielekezwe taratibu za nini ninapaswa kufanya kutokana na tatizo la kitaaluma lililonipata. Nilikuwa mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Mtakatifu Agustino(SAUT) katika mojawapo ya matawi yake yaliyopo nchini tangu mwaka 2010.Katika miaka miwili ya mwanzo yaani mwaka 1&2 nilifanikiwa kukamilisha malipo yote ya ada.Lakini katika mwaka wa tatu wa masomo nilishindwa kukamilisha malipo yote ya ada na hivyo nikazuiwa kufanya mitihani yangu ya mwisho.Kufuatia hali yangu mbaya ya kiuchumi kwa sasa sioni uwezekano wa kupata kiasi cha pesa ninachodaiw ili nikafanye special exams 23 sept 2013.Je ktk mazingira haya ambayo nimna matokeo ya semester tano,nifanyeje? naombeni ushauri wenu wanajamvi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…