Naombeni ushauri mie, nimeaibika sijui nitauficha wapi uso wangu

Song of Solomon

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2021
Posts
2,752
Reaction score
5,609
Mke wangu alichukua simu yangu na kufuta namba ya mpenzi wangu mwingine, namba ya Magreth na kuhifadhi namba yake ya kuwa anaitwa Magreth.

Sikujua kuwa kuna mtu alimwambia mke wangu kuhusu Magreth, kisha nikapokea SMS kutoka kwa Magreth akiomba pesa Sh.250,000.

Nilimkimbilia mke wangu kwa kuwa sikuwa na hiyo hela wakati huo na kumdanganya kuwa nahitaji Sh. 250,000 kwa dharura. Nilimwambia kuwa mdogo wangu Rutta anaumwa na anahitaji pesa haraka.

Mke wangu alinipa zile pesa na nikakimbilia kutuma kwenye akaunti namba iliyoandikwa kwenye ule ujumbe.

Nikiwa nimejipumzisha nyumbani baada ya kutoka kazini, niliendelea kuwaza iwapo Magreth alipokea pesa hizo.
Nilimtumia SMS ili kujua kama alikuwa amepokea pesa. Jibu lake lilikuwa, "Nipigie sasa."

Nilitoka nje nyuma ya nyumba kupiga simu.
Weeeeeeh!

Unaweza kufikiria uso wangu wa kutisha ulivyokuwa niliposikia sauti ya mke wangu badala ya Magreth!
Leo ni siku ya tatu bado nimesimama nje.

Sijui jinsi ya kurudi nyumbani kwangu !!!

Ushauri wowote tafadhali [emoji53]...
 
Punguza sukari kwenye hiyo chai.

1- "Leo ni siku ya tatu bado nimesimama nje". Kitu ambacho ni uongo wa kiwango cha Lami inamaana hua haulali siku zote hizo?

2,3,4,5,...- eti unakurupuka kutuma je, kama ni utapeli na je hukukalili hata namba pindi unapiga kua hiyo si yake? Yaani hujui kutofautisha namba ya mke na mchepuko.
Mengi umetupiga kamba.
 
Mkuu huon kwamba hiyi stori umeikopi sehemu?

Je ni mwanaume Boga kiasi gani atatuma pesa bila kuhakiki namba?

Ni uchiz kias gani mpaka jina la mkeo na mchepuko kushinda kutofautisha kwenye hizo mpesa

Maswali ni mengi ila[emoji116][emoji116]View attachment 2032509

Sent from 2 using JamiiForums mobile app
Uhuni
Anatuona wote wasenge humu ndani
 
Mke wangu alichukua simu yangu na kufuta namba ya mpenzi wangu mwingine, namba ya Magreth na kuhifadhi namba yake ya kuwa anaitwa Magreth.
Sikujua kuwa kuna mtu alimwambia mke wangu kuhusu Magreth, kisha nikapokea SMS kutoka kwa Magreth akiomba pesa Sh.250,000.
Nilimkimbilia mke wangu kwa kuwa sikuwa na hiyo hela wakati huo na kumdanganya kuwa nahitaji Sh. 250,000 kwa dharura. Nilimwambia kuwa mdogo wangu Rutta anaumwa na anahitaji pesa haraka.
Mke wangu alinipa zile pesa na nikakimbilia kutuma kwenye akaunti namba iliyoandikwa kwenye ule ujumbe.

Nikiwa nimejipumzisha nyumbani baada ya kutoka kazini, niliendelea kuwaza iwapo Magreth alipokea pesa hizo.
Nilimtumia SMS ili kujua kama alikuwa amepokea pesa. Jibu lake lilikuwa, "Nipigie sasa."
Nilitoka nje nyuma ya nyumba kupiga simu.
Weeeeeeh!
Unaweza kufikiria uso wangu wa kutisha ulivyokuwa niliposikia sauti ya mke wangu badala ya Magreth!
Leo ni siku ya tatu bado nimesimama nje.
Sijui jinsi ya kurudi nyumbani kwangu !!!

Ushauri wowote tafadhali [emoji53]...
Nikiwa sebleni kwa shemeji yangu na king'amuzi ameshakilipia huku na subiri dada apike ugali na nyama nile.....Mwambie shetani alikupitia mkaondoka naye ndio unarudi sasa
 
Ukiskia kimeumana ndo Hii Sasa....

Una MKE smart Sana, anastahili pongezi[emoji1787]
 
Mkuu huon kwamba hiyi stori umeikopi sehemu?

Je ni mwanaume Boga kiasi gani atatuma pesa bila kuhakiki namba?

Ni uchiz kias gani mpaka jina la mkeo na mchepuko kushinda kutofautisha kwenye hizo mpesa

Maswali ni mengi ila[emoji116][emoji116]View attachment 2032509

Sent from 2 using JamiiForums mobile app
Uhuni
Hii itakua chai aisee[emoji1787]
 
Mke wangu alichukua simu yangu na kufuta namba ya mpenzi wangu mwingine, namba ya Magreth na kuhifadhi namba yake ya kuwa anaitwa Magreth.
Sikujua kuwa kuna mtu alimwambia mke wangu kuhusu Magreth, kisha nikapokea SMS kutoka kwa Magreth akiomba pesa Sh.250,000.
Nilimkimbilia mke wangu kwa kuwa sikuwa na hiyo hela wakati huo na kumdanganya kuwa nahitaji Sh. 250,000 kwa dharura. Nilimwambia kuwa mdogo wangu Rutta anaumwa na anahitaji pesa haraka.
Mke wangu alinipa zile pesa na nikakimbilia kutuma kwenye akaunti namba iliyoandikwa kwenye ule ujumbe.

Nikiwa nimejipumzisha nyumbani baada ya kutoka kazini, niliendelea kuwaza iwapo Magreth alipokea pesa hizo.
Nilimtumia SMS ili kujua kama alikuwa amepokea pesa. Jibu lake lilikuwa, "Nipigie sasa."
Nilitoka nje nyuma ya nyumba kupiga simu.
Weeeeeeh!
Unaweza kufikiria uso wangu wa kutisha ulivyokuwa niliposikia sauti ya mke wangu badala ya Magreth!
Leo ni siku ya tatu bado nimesimama nje.
Sijui jinsi ya kurudi nyumbani kwangu !!!

Ushauri wowote tafadhali [emoji53]...
Acha fix jina la mkeo hukuliona kwenye muamala?
 
Back
Top Bottom