Naombeni ushauri 'Mini car' gani ya kununua

Naombeni ushauri 'Mini car' gani ya kununua

Hechinodemata

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2016
Posts
1,488
Reaction score
3,338
Habari za jioni wana JF,

Kwa zingatia hali halisi ya mazingira nimejibanabana katika mihangaiko yangu ya muda mrefu nimepata fedha kiasi fulani cha kununua kagari ka kutembelea ili kanisaidie mimi na familia yangu ya watu 4.

Naombeni uzoefu wenu juu ya hizi mini car. Je ni magari yapi ni imara na yanatumia mafuta kwa kiasi kidogo na spare zake zinapatikana kwa urahisi?

Natanguliza shukrani kwa ushauri
 
Nahitaji ushauri kaka pesa sio tatizo sana

una uhakika? maana sio kwa maneno haya...

nimepata fedha kiasi fulani cha kununua kagari

Haya bana..ushauri wangu kanunue AUDI kati ya A1 - A3

uchumi ukibana..nunua COOPER

ila wewe kwa mbwembwe zako nunua tu VITZ ukitaka durability tafuta STARLET Zenji benji nzuri kabisa...
 
una uhakika? maana sio kwa maneno haya...



Haya bana..ushauri wangu kanunue AUDI kati ya A1 - A3

uchumi ukibana..nunua COOPER

ila wewe kwa mbwembwe zako nunua tu VITZ ukitaka durability tafuta STARLET Zenji benji nzuri kabisa...
asante, starlet cc ngapi, zenji nazipataje nomba ufafanuz
 
Mtoa mada kuandika bageti yako ni kitu muhimu sana ili watu wakushauri. Hizo gari min imara na zinazokula mafuta vizuri,unaweza pata kuanzia m8 hadi m90.

Nakukadiria bajeti yako ni kati ya m8 hadi m12
1) Toyota carina Ti
2)Vw gulf
3)Toyota ist
4)Toyota Raum
5)Toyota rav4 chini ya mwaka 1999 na iwe milango mitatu.

Waliokushauri kuhusu passo nachelea kusema ni gari nyepesi sana kwa barabara zetu inachakaa mapema.

Kuhusu starlet ni kweli ni gari imara ila sikushauri ununua mana hizi gari zimesimamishwa kutengenezwa muda mrefu sana hivo spea zake hususani upande wa bodi ni adimu kidogo.
 
Mkuu,kwa vigezo vyako naona options ni hizi;
1. Toyota Rush (1490cc)
2. Suzuki Jimny (660cc) -za kuanzia mwaka 2000+
3. Mitsubish Pajero mini (660cc) -za kuanzia mwaka 2000+
 
Back
Top Bottom