Naombeni ushauri: Mwenyekiti ananisumbua katika biashara yangu

jacobcm8

Senior Member
Joined
Apr 10, 2014
Posts
173
Reaction score
122
Mimi ni mwanachuo mwaka wa tatu (BscCIM) pia Mfanyabiashara nmejitahidi kupambana na maisha nikafungua ofisi yangu ninayochezesha GAMES ZA WATOTO JAPO HATA WAKUBWA UNACHEZA TU (PLAYSATION 4) ila leseni ya biashara imeandikwa michezo ya watoto pia natengeneza computer simu etc.

Kuna changamoto kubwa ninayokumbana nayo ni kuna uyo mzazi alinifuata akaniambia hataki mtoto wake ajihusishe na kucheza games ofisini kwangu nikamzuia kabisa na mtoto hajawahi kuja tena, kumbe mtoto anaenda kucheza games ofisi za mbali zaidi ila lawama zote nakuja kubeba mimi wa karibu.

Sasa kuna huyo Mwenyekiti wa Mtaa leo kaja kafukuza watu wote ofisini kwangu (wateja) sikuwepo mda huo ila nimeambiwa hataki mtoto yoyote mda wowote ule lakini leseni inasema ni michezo ya watoto.

Sasa nimekaa nimefikiri nataka nimfungulie kesi ya kumshitaki analeta fujo kwenye biashara maana alikuja mara mbili na zote ikiwemo ya leo amelewa pombe na amefukuza wateja lakini ile sio biashara haramu maana Tanzania nzima zipo nyingi tu hizi game senta.

Nafikiri nilete kijana nitakae mwajiri sasa akikutana na changamoto kama hizi itakua ni tatizo maana mimi naingia field hapo mwezi wa 10 na nitakua field semister nzima.

So nafikiri nimshitaki uyu mzee mlevi ashike adabu na biashara za watu tra nalipia kodi mimi. Leseni ninayo afisa biashara kanipa. Sasa sielewi shida ipo wapi.

Naombeni ushauri huyu mzee mwenyekiti nikamripoti
? maana nahisi naonewa katika hili
 
Mkuu kabla ya kumpeleka katika vyombo vya sheria hakikisha umeongea nae vizuri..akikaidi ndio uchukue hatua zaidi..

Usikubali akuharibie malengo yako, umeamua kujiajiri halafu aje tu akuharibie

Uzuri mmoja vibali vyote unavyo
 
kabla ya kumshtaki, beba leseni yako ya biashara mfate ofisini kwake kampe onyo kuwa anakuzuiya wewe kulipa kodi ya serikali unayoilipa kihalali kwa biashara hiyo halali,

akirudia tena kata RB weka ndani bazazi huyo na useme siku ya tukio alikimbia na droo ya pesa za mauzo.
 
Pole sana
"Kadri unavyopanua ndivyo watu wanazidi kutamani"

By Anna tibaijuka pesa ya mboga
Ahsante ndugu kwa kweli hii ni changamoto kubwa kwangu ukizngatia malengo ni fungue ofs ingine kama hii sehemu ingine ili kuongeza income per day....
 
Mshikishe adabu huyo Zombie akome ubishi mamayo zake! Pia kama na ww unaonyesha pilau kwa watoto Mkuu au watoto wanatoroka shule then wanakuja kuangalia hzo games ujitahd kuwa makini
 
Huyo mwenye kiti na njaa kali sana hana Kingine ukiona vipi mtoe ya gongo atatulia lakini kuwa makini asizoee
Boss na ni njaa kweli anayo ........mm ningemtoa kama ingekuwa biashara haramu..... pia akiishiwaga atakua ananizoea zoea anajua pa kupiga pesa papo..hufanya ivo kwa wengine

Ananizingua mm akati mtoto wake kashndwa kumlea anavuja bangi , Sigara anavuta pakti kadhaa per day.... nasndwa kumuelewa kabsa yan uyu mzee.
 
Kabla ya kwenda hakikisha unahakika ya Ku control watoto washule wasije kucheza gemu zako wakati masomo yanaendelea. Hapo ndipp nahisi huyo Mzee anaweza kukushindia.
 
Mkuu kabla ya kumpeleka katika vyombo vya sheria hakikisha umeongea nae vizuri..akikaidi ndio uchukue hatua zaidi..

Usikubali akuharibie malengo yako, umeamua kujiajiri halafu aje tu akuharibie

Uzuri mmoja vibali vyote unavyo
Kweli mkuu nitafanya kumtafuta leo ninapata asira kuona mtu anaweka vikwazo issue ambayo ina uhalali 100%

Na nikichek hustle nazopitia si kitoto mtu anachukulia easy tuu......

[HASHTAG]#akikaidi[/HASHTAG] hatonisahau ....
[emoji120]
 
atazoea tuu akiishiwa atafuata tena apo ni kumkata mapema
Kweli boss ndio mchezo wa huyu mzee......icho kitu awajaribu wengine hustle nlizopitia kufika nlipo siezi toa ela kipuuuzi mm....bora nitoe msaada ...
Au angenifata direct anambie anashida na pesa ningempa sio kutumia cheo chake kutukandamiza amefail..[emoji120]
 
Kabla ya kwenda hakikisha unahakika ya Ku control watoto washule wasije kucheza gemu zako wakati masomo yanaendelea. Hapo ndipp nahisi huyo Mzee anaweza kukushindia.
NOW NI LIKIZO Halafu siku za shule uwaga wanakuja saa 9 huko baada ya kutoka shule .....
Wateja wangu wakubwa ni wanachuo...hao watoto nipo nao makini huwa nawaambiaga wasome shule wafike nilipo..........
''Yeye anadai marufuku mtoto kuonekana muda wowote''' hata weekend anazinguaga.....kuna iyo siku aliwakuta wanachuo wenzangu walimzingua mno akakimbia....
 
Mshikishe adabu huyo Zombie akome ubishi mamayo zake! Pia kama na ww unaonyesha pilau kwa watoto Mkuu au watoto wanatoroka shule then wanakuja kuangalia hzo games ujitahd kuwa makini
Okay boss watoto kutoroka shule na kuja hapa ni ngumu sababu ofsi ipoo sehemu ya wazi hivo kushtukiwa rahisi.... afu watoto siku za shule huja saa 9 nakuendelea after shule........
 
Kweli mkuu nitafanya kumtafuta leo ninapata asira kuona mtu anaweka vikwazo issue ambayo ina uhalali 100%

Na nikichek hustle nazopitia si kitoto mtu anachukulia easy tuu......

[HASHTAG]#akikaidi[/HASHTAG] hatonisahau ....
[emoji120]
Poa mkuu ulete mrejesho..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…