everythinggoes
Member
- Dec 27, 2012
- 13
- 2
Habari zenu wadau, nina imani mnaendela vizuri na msimu huu wa sikukuu za xmas na mwaka mpya wa 2013.
kama kichwa na cha habari kinavyosema hapo juu naombeni msaada kwa wenye ujuzi hasa doctors. Pia ningependa tu kusema kuwa issue hii inanihusu mimi binafsi na wala sio jirani rafiki wala ndugu. (wengi kwa kuficha aibu hupenda kusema kuna rafiki/ndugu yangu anataka ushauri).
Mimi niko kwenye mid-fourtees sasa hivi, kwa bahati mbaya au nzuri sikuwahi kufanyiwa tohara na wazazi wangu, kusema kweli sijui kama sababu ni imani au kitu gani, mimi ni mkristo na sikuwahi kuuliza na hata nikitaka kuuliza kwa sasa, baba yangu hayupo sasa hivi ameshatangulia mbele za haki.
Nina mke, mke wangu hajawahi kuonesha kukoseshwa raha na hali hii, nakumbuka mara ya kwanza ku do nilimwambia status yangu na alisema hiyo sio issue kwake. Tumekuwa pamoja for almost ten years now.
Kinachonifanya nilete hii case hapa ni kuwa sasa ningependa kufanyiwa tohara. niongeze tena kuwa sijawahi kupata tatizo lolote la kiafya kutokana na hali yangu.
Sasa maswali yangu ni kama ifuatavyo.
1. Kwa umri huu ni sawa kufanyiwa tohara au nimechelewa?
2. Kama inawezekana, ni wapi (Dar es Salaam) naweza kupata huduma hii kukiwa na usiri ili kulinda heshima yangu?
3. Huduma hii itanigharimu shilingi ngapi na ni process ya muda gani? nina maana muda wa operesheni/muda wa kupona.
4. Je, kuna mabadiliko yoyote nitayapata katika maisha yangu ya sex?
kwa sasa ni hayo tu wandugu, ninaamini majibu kwa swali langu yanaweza pia kusaidia wengine wenye mawazo kama yangu. Hivyo nategema staha katika michango yenu ingawa pia niko tayari kuvumilia aina yoyote ya majibu nikiamini hii ni hali ya muda mfupi tu, na shida yangu ya msingi ni kupata ushauri wenu waungwana.
NB: nimeshafanya utafiti google na kupata majibu mengi tu tofauti tofauti, ila sasa ninataka kupata ushauri kutoka kwa ma doctor wangu wa jf.
Asanteni sana.