Naombeni ushauri, Nimejitahidi sana kuwa na moustache bila mafanikio

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
Wadau wa JF

Hamjamboni?

Kwa muda mrefu nimejitahidi sana kuwa na muonekano wenye moustache bila mafanikio.

Umri wangu kwa sasa unasonga mbele kwa kasi lakini sijona mafanikio yeyote zaidi ya kuwa na masharubu Urefu wangu ni ni futi 6 na uzito wa kg 92 nikiwa na rangi nyeusi.

Kwa heshima kubwa naombeni ushauri wenu.

Aksanteni sana
 
Duh, pole, mwonekano wa mwili hutengenezwa na vinasaba ambavyo hurithishwa kutoka kizazi kimoja kwenda kingine, kama kwenye vinasaba vyako ulivyorithi kutoka kwa wazazi wako hakuna kinachoweza kuleta mwonekano huo, ni vigumu, huo ndio uelewa wangu nikirejelea somo la genetics na heredity sijui ilikuwa kidato cha nne kama sijasahau
 
Dah, Wengine yanatukera yalivyokuwa mengi hayo masharafa
 
Wazungu waliamini mustache huwapata MATAJIRI na ilikuwa kama Kweli
 
Mambo ya Walawi 19:27 Msinyoe denge pembe za vichwani, wala msiharibu pembe za ndevu zenu.
 
Nenda Kaole.Wanaweza kukushauri maana waigizaji wana namna nyingi ya kubandika nywele za mahali popote.
 
Mkuu ungeweka picha ingekua powaa....tukapata pa kuanzia....
 
Dunia ina mambo, vile me sipendi kiwa na hii makitu eti kuna mtu anatamani. Bro hata ukiwa nayo haya kama huna mvuto huna tu.

Tafuta hela hizo sharubu zinajiotea zenyewe tu
 
Una umri gani?
 
Matola nimeku pm.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…