Naombeni ushauri nimemfumania shemeji yangu

Naombeni ushauri nimemfumania shemeji yangu

Joined
Dec 11, 2020
Posts
60
Reaction score
157
Habari Wana jamvi,

Kama kichwa kinavyojieleza hapo juu.

Nina rafiki yangu ambaye ni Kama ndugu yangu kwa jinsi tunavyoishi na kusaidiana once changamoto za kimaisha zinapo arise.

Nimeishi vizuri Sana na huyu rafiki yangu tena kwa ukaribu Sana tukiwa mtaa mmoja. lakini kwa Sasa tupo mbali kwa maana ya distance lakini urafiki wetu bado upo na unakua siku Hadi siku.

Huyo rafiki yangu ni mtumishi wa taasisi Y wakati mke wake naye ni mtumishi wa taasisi W (mwanamke ni mtu wa kusafiri Mara kwa Mara kwa nature ya kazi yao).

Sasa week chache zilizopita nikiwa kwenye Moja ya group la WhatsApp linalodeal na ndoa.

Ghafla nikaona picha ya Shemeji yangu akiwa huged na jamaa Fulani imetumwa kwenye group na jamaa.

Kwa Sababu namfaham nilishtuka Sana nikafuatilia vizuri nani ametuma Ile picha, nikapata kumfaham. nikiwa najiuliza maswali na kutafakari.

Moja ya member katika hilo group aliuliza kwa kumtag mtu aliyetuma Ile picha,,, Boss huyo mwanamke ni mkali Sana ni wa wawapi...?

Jamaa akajibu ni wa mkoa X, alipo taja mkoa kwangu maumivu makali Sana yalikuwa upande wangu as if Mimi ndiye nasaritiwa.

Why niliumia Sasa Mimi wakati sio mke wangu amefanya hivyo?

Kama nilivyosema awali mume wa huyo mwanamke ni rafiki yangu Sana na tumepitia mengi Sana pamoja so ni Kama ndugu yangu tu kwa Sasa.

Huyo Shemeji kabla ya kuwa na rafiki yangu alikuwa na mahusiano na jamaa mmoja ambaye alikuwa na kesi. Yule jamaa akamkopa mwanamke pesa akimuahidi atamrudishia kumbe dhamira yake ni kumtapeli mwanamke na kweli mwanamke alikopa pesa kwenye Vikoba na akachukua mkopo benk then akampa jamaa apeleke kwenye kesi aliyokuwa anakabiliwa nayo.

Kumbe jamaa alifake na kutengeneza matukio ili apate pesa Wala hakukuwepo na kesi halisia Bali ilikuwa ni mipango iliyofanywa na Wakili asiyekuwa mwaminifu.

Basi mgogoro mkubwa ukaibuka mpaka mahusiano yakavunjika.

Ndipo huyo mwanamke akaanza mahusiano na rafiki yangu, kwa Sababu rafiki yangu ni ndugu yangu the way tulivyishi akamtambulisha kwangu yule mwanamke then maisha yakaendelee.

Ila kabla hatujua kuwa mwanamke alikotoka alikuwa na mzigo wa mikopo.

Kuna siku nilimuuliza rafiki yangu unaijua background ya huyo mwanamke ? Akasema hapana hakujua nilimshauri afuatilie kweli anagundua kuwa mwanamke yupo single kwa siku 25.

Hiyo taarifa ilinishtua kidogo na kunipa maswali inawezekanaje mwanamke aliyeumizwa Sana hajapata muda wa kutafakari anaanzisha mahusiano mapya ndani ya muda mfupi hivyo?

Seriously nilihisi hapo Kuna kitu zaidi kinatafutwa sio upendo, nikutaka kumhoji Sana rafiki yangu nilimwambia tu awe makini sana, Basi maisha yakaendelea Kama kawaida.

Miezi kadhaa badaye nikaona rafiki yangu anahangaika Sana kutafuta pesa ikionyesha ana uhitaji mkubwa Sana wa pesa isivyo kawaida yake.

Kama tujuavyo ukitaka kumjua mtu kaa karibu naye so kwa ukaribu niliokuwa nao kwa rafiki yangu niligundua jamaa ana matatizo.

Nikaomba kuongea naye bila hiana akafunguka yote A to Z kuhusu Shemeji na mikopo aliyochukua benk na kwenye vikobo ilikuwa mikopo iliyokuwa kiasi kwamba mshahara wote ulikuwa unakatwa huko huko, huku wa Vikoba nao wakiwa wanamsumbua sana.

Basi nikaingiwa na hurumu Sana kumuona rafiki yangu anateseka vile Kuna kiendo tulinunua eneo la pamoja kwa lengo la kujenga fremu za biashara Kisha tugawane fremu.

Rafiki yangu akaniomba kuuze ili ipatikane pesa ya haraka kuclear mikopo ya Shemeji.
nampenda Sana rafiki yangu, nilikubali kufanya hivyo.

Tukauza tukaclear mikopo yote ya Shemeji maisha yakaendelee.

Mimi nikapata Safari ya kikazi kwenda nje ya Tz. Wakati nasafiri rafiki yangu alikuwa kwenye process za mwisho kabsa za kumuoa huyo Shemeji yangu.

MUNGU saidia kweli alifanikisha na Mambo yalienda vizuri kabisa thou niliumia kutohudhuria harusi ya rafiki yangu lakini sikuwa na namna majukumu ya kazi yalinibana Sana.

Yapata miaka miwili Sasa sijaonana live na rafiki yangu japo tunawasiliana vizuri na Kama Kuna changamoto tunashirikishana ingawa Kuna mazingira nakuwa nipo mawasiliano yanakuwa hamna kabisa mwezi mzima au zaidi.

Mpaka hapa mtakuwa mmeelewa kwanini naumia Sana kuona huo usariti.

Sasa turudi kwenye group la WhatsApp,

Baada ya kuona Ile picha ya mke wa rafiki yangu nikataka evidence juu ya lile Jambo, kweli nilipata evidence zote zikiwemo videos.

Kumbe Mwanamke anamuaga Mwanume kuwa waenda kikazi kwenye mkoa huo lakini kumbe anaenda kwa mwanaume mwingine(mchepuko).

Kusema kweli tangu nione usariti ule nimejikuta sipo sawa kabisa naumia Sana maana rafiki yangu amehangaika Sana na kuhairisha Mambo yake mengi ili tu kuweza kumsaidia mwanamke pamoja na familia ya mwanamke.

Hapa napambana na nafsi mbili

Moja inaniambia nimwambie rafiki yangu ....na nafsi nyingine inasema nisimwambie ...

Tafadhali naombeni ushauri wenu wana jamvi nifanye nini nampenda Sana rafiki yangu

Nakuja kwenu kupata ushauri mpana zaidi.
 
Habari Wana jamvi,
Kama kichwa kinavyojieleza hapo juu.

Nina rafiki yangu ambaye ni Kama ndugu yangu kwa jinsi tunavyoishi na kusaidiana once chang

Naona utumie busara kumwambia amchunguze mkewe na safari zake ila usimwambie direct. Kama anampenda sana mke wake anaeza akaona unamsingizia na hata ukionyesha ushahidi mwanamke anaweza jitetea ukaonekana mbaya…mapenzi yana ufala mwingi, maandiko matakatifu ya biblia yanasema Ndoa na iheshimiwe na watu wote…usiwe chanzo cha kuvunjika kwa ndoa ya watu.
 
Mwambie rafiki yako, hakikisha unampa na ushahidi.
Lakini pia jiweke kwenye utayari wa kuvunjika kwa urafiki wenu. Na kama rafiki yako hato kuelewa, I'm sure kuna tatizo ama usaliti atakuja gundua kwa mkewe na hapo ndipo atakapo juta na kujikuta amepoteza rafiki na mke
 
Nakushauri ukakabe nafasi ya huyo shemeji yako.

Usikubali kabisa ujinga wahi fasta kamwambia mumewe ili uzibe hilo pengo litakalojitokeza
 
uphaller mwingine,

kosa la kwanza mwanamke kaisaliti ndoa yake, kosa lingine kubwa zaidi ni kwenda kumsaliti mumewe kwa takataka moja isiyojielewa inayopost picha za ushahidi pamoja na video kwenye group, huku ikijua kabisa huyo ni mke wa mtu (hata ingekuwa hajaolewa bado siyo busara)..!

Watakushauri wenye busara zao mingi, me nimemaindi tu vile hao wachepukaji wote ile namna hawajielewi, mtseeeuuw' zao...!
 
Tafuta admin au mtu yoyote amuunganishe katika Hilo kundi la whatsaap then wewe nitoe kwa siku chache kama mbili Tatu hivi halafu hizo picha azione basi hapo jamaa atajua kila kitu na baadae atolewe na wewe urudi. Hatajua kama wewe ni mhusika ila atajua yote na ushahidi. Mke hapo atajua afanye nini
 
Kuna siku nilimuuliza rafiki yangu unaijua background ya huyo mwanamke ? Akasema hapana hakujua nilimshauri afuatilie kweli anagundua kuwa mwanamke yupo single kwa siku 25.
Siku hizi mnapangwa arithmetically hata watano at a time na mmoja akiachia ngazi/akitupwa kule, wengine wanne wanaendelea. Wewe unashangaa siku 25 zote hizo?
 
Kama ni mimi simwambii lolote juu ya hilo hadi mhusika mwenyewe atakapolitambua hilo yeye mwenyewe kwakuwa ni mke wake wa ndoa.

Hukumu za mambo ya ndoa huwa ni ngumu sana sana sana
Labda tumetofautiana huyu ni rafiki yangu zaidi ya ndugu tumetoka mbali Sana ndio Maana naumia Sana mpaka naomba ushauri zaidi means nashindwa kulibeba kimya kimya.
 
Mwambie rafiki yako, hakikisha unampa na ushahidi.
Lakini pia jiweke kwenye utayari wa kuvunjika kwa urafiki wenu. Na kama rafiki yako hato kuelewa, I'm sure kuna tatizo ama usaliti atakuja gundua kwa mkewe na hapo ndipo atakapo juta na kujikuta amepoteza rafiki na mke
Je nikimwambia kwa njia ya simu Ina Afya au nionane naye ana kwa ana....???
Maana kwa Sasa nipo mbali naye kwa Maana ya distance.
 
Back
Top Bottom