Naombeni ushauri wa kisheria ili niwe na amani

Naombeni ushauri wa kisheria ili niwe na amani

mtk eng

Senior Member
Joined
Oct 18, 2021
Posts
103
Reaction score
237
Iko hivi.. kuna kiwanja nimenunua muuzaji kanionesha ramani ambayo imechorwa na surveyor wake ..madai yake kasema alienda ofisi za ardhi kujua eneo analotaka Kuuza ni kwaajil ya makazi au limetengwa kwaajili ya shughuli za serikal na akapata majibu kua eneo ni kwaajil ya makazi.. alichokifanya muuzaji ni kumuita surveyor wake na akamcholea mchoro na ukaonesha unatoa viwanja 8 na vyenye ukubwa wa square meters 500 each one.. na mimi nikafanikiwa kuchukua kimoja.. na tukaandikishana kwa ofisi za kata.. swali langu jee naweza nikaanza ujenzi? Pili je kiwanja kiko salama? Nifanyeje naombeni ushauri wa kitaalamu nisije niingiazwa mkenge..
Screenshot_20220122-014319_WhatsApp.jpg
 
Sasa kama umeshanunua unataka ushauri gani tena?ww subiri yajayo kama yatakwepo upambane nayo.

Unachukua chakula unakula halafu unauliza kama kiko salama au VP? Sasa ukiambiwa hakiko salama itasaidia nn wakati umeshakula tayari??

Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app
Yan hapo nauliza ili nipewe ushauli wa kitaalamu ili niutumie katika hilo.
 
Iko hivi.. kuna kiwanja nimenunua muuzaji kanionesha ramani ambayo imechorwa na surveyor wake ..madai yake kasema alienda ofisi za ardhi kujua eneo analotaka Kuuza ni kwaajil ya makazi au limetengwa kwaajili ya shughuli za serikal na akapata majibu kua eneo ni kwaajil ya makazi.. alichokifanya muuzaji ni kumuita surveyor wake na akamcholea mchoro na ukaonesha unatoa viwanja 8 na vyenye ukubwa wa square meters 500 each one.. na mimi nikafanikiwa kuchukua kimoja.. na tukaandikishana kwa ofisi za kata.. swali langu jee naweza nikaanza ujenzi? Pili je kiwanja kiko salama? Nifanyeje naombeni ushauri wa kitaalamu nisije niingiazwa mkenge..View attachment 2091005
Kwenye ununuzi wa aridhi kuna kanuni moja inasema mnunuzi kuwa makimakini (buyer be ware). Wewe mnunuzi ndio unawajibu wakufanya utafiti kabla yakununua eneo kwenye ofisi za aridhi wilaya/mkoa ili kujiridhisha juu ya matumizi sahihi ya eneo husika napia kujua nani hasa nimmiliki halali wa eneo usika.

Kufanya uchunguzi wa muonekano wa eneo husika, linapakana na nani nk. Linamgogoro wowote ama laa.

NB: MTU anaepaswa kusimamia mchakato wa uuzaji na ununuzi wa eneo lililopimwa ni mwanasheria(wakili), hii nikwasababu yeye anafahamu taratibu zote za kisheria na namna mikataba inavyotakiwa kuwa ya ununuzi wa aridhi.

Chakusikitisha umekumbuka kunawa baada yakuanza kula, hivyo hatua zote za msingi ulizopaswa kuzifwata kabla ya ununuzi wa eneo umeziruka.

UNAWEZA KUWASILIANA NA MWANASHERIA WAKO ILI KUJUAZAIDI HATUA GANI MNAWEZA KUZICHUA.
 
Umepewa risiti ya mashine? Umenunua kwa jina la kiwanja au kwa jina la shamba?
 
Ninachokiona Ni kuwa eneo limepimwa lakini halijapewa hati. (Certificate).
Kwahiyo pata uhakika Kama eneo Hilo Ni kwa ajili ya makazi Kama ndio. Fanya utaratibu wa kupata hati toka afisi ya ardhi.
Kwa sasa hakikisha mamlaka za serikali ya mtaa zimethibitisha mkataba wenu, pamoja na majirani unaopakana nao.

Kwa maoni yangu ukishajua eneo Hilo Ni la makazi, si vibaya ukaanza Mara moja ujenzi, Ila ukachukue kibali Cha ujenzi toka serikali za mitaa. Hii itasaidia jamaa kuja kukugeuka.

Hongera Sana kwa kununua ardhi.
 
Ninachokiona Ni kuwa eneo limepimwa lakini halijapewa hati. (Certificate).
Kwahiyo pata uhakika Kama eneo Hilo Ni kwa ajili ya makazi Kama ndio. Fanya utaratibu wa kupata hati toka afisi ya ardhi.
Kwa sasa hakikisha mamlaka za serikali ya mtaa zimethibitisha mkataba wenu, pamoja na majirani unaopakana nao.

Kwa maoni yangu ukishajua eneo Hilo Ni la makazi, si vibaya ukaanza Mara moja ujenzi, Ila ukachukue kibali Cha ujenzi toka serikali za mitaa. Hii itasaidia jamaa kuja kukugeuka.

Hongera Sana kwa kununua ardhi.
Shukrani mkuu
 
Back
Top Bottom