Naombeni Ushauri wa kisheria juu ya Mafisadi hawa.

ELIBARIKI SARUNI

New Member
Joined
Mar 11, 2012
Posts
4
Reaction score
0
Ndugu zangu wana jamii wenzagu mimi ninahitaji ushauri katika hili Kata yangu toka mimi nimezaliwa nimesimiliwa mpaka nimekuwa mkubwa sasa ninaona kwa macho yangu mwenyewe watu wanavyo jichotea pesa za serikali zinazoelekezwa ndani ya kata na pia kufanya michango holela kwa kuwalazimisha wananchi kuchangia na kuingia mtini.

Sasa iliyotuacha hoi lkn vilevile sio jipya kutokea ni PEMBE JEO ZA KILIMO, zipo taratibu elekezi za kufuata kabla ya kugawa kwa wananchi lkn ajabu zote zilikiukwa walichagua kamati wenyewe kwa kuteuna badala ya kuitisha mkutano wa wananchi kama taratibu zinavyoelekeza lkn pia cha ajabu zaidi pembejeo hizi ziliuzwa kwa wananchi kwa SH 8,300/= Pamoja na kuchukua mbolea ya kupandia na kukuzia eti Kama unataka kuchukua mbolea itakulazimu uchangie SH 80,000 vinginevyo utalazimika kuchukua mbegu tu.

Lakini pia kutokana na ugumu wa maisha ya Mtanzania wa kawaida wa sasa atatoa wapi hiyo pesa? ni bora achukue Mbegu auze kilo mbili apate Sh 8,300/= ya Wakala atemane na mbolea kama vp? Mungu asaidie huko shambani. Michango mingine mingi ziliingizwa mtini, kama pesa za ujenzi wa sekondari ni takribani miaka 3 sasa toka wananchi wachange pesa za ujenzi pomoja na ya maji SH 10,000 @ mwananchi na Hakikazi nao waliwatia moyo wananchi kwa kuwachangia SH 9,000,000/= lkn mpaka leo ilishakuwa hadithi tu.

Ilikuwa kazi ngumu sana lkn juhudi sasa zinaweza kuzaa matunda Tulimweleza Mh: Godbless Lema (Mb) kutokana na mizi kuwa mikubwa na ya mda mrefu walikuwa wanakana mambo yaliyokowazi mbele ya wananchi na Mhe: DC lkn ni kwa maneno tu Vitabu vile vya vocha walisaini wenyewe tena kabla ya zoezi kuisha tayari walikuwa wamekwisha sain vitabu vyote kwa niaba ya Wananchi.

Sasa tukiachilia mbali hayo yote Wananchi walishapoteza imani na Uongozi wa Kata wote kwa ujumla na wanataka kuwaondoa wote Je? Ndugu zangu taratibu zitakazo fanikisha swala zima ni zipi?
 
Unaposema mnataka kuwang'oa hao viongoz jitahid kuwa specific, maana kata inaendeshwa na WDC ambayo m/kiti wake n diwani,katibu ni afisa mtendaji kata, na wajumbe wake n wenyeviti wa mitaa/vjiji.
Na kila mmoja ana utaratibu wake wa kumuondoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…