Hili suala la kukosa wazo la nini cha kufanya naweza kusema ni Ugonjwa.
Na ugonjwa huu unaathiri saana vijana wa mjini na sio vijijini na baadhi ya mikoa.
Na Zaidi hutokana na vijana kutokujitambua na zaidi kusubiria mtu apate pesa ndio afikirie cha kufanya,wakati inatakiwa kuanzia miaka 8 yaani utoto lazima uwe na kitu unachopenda kufanya licha ya kwamba umri unavyozidi kwenda unazidi kuweka mizizi ya wazo laki na hata uki change basi una change for the best baada ya kujifunza.
Najingine ni vijana kukimbia kujitolea kwa wenye biashara husika,kuna watu wanabiashara zao unaweza kwenda kufanya hata kwa kulipwa kidogo ili ujifunze,ila kila kijana kwa hili hataki,yeye ni kuuza suraaa kwenda mbele,kukesha na sim kama kombaaa
Kwa ufupi nenda kwenye sticky post hapo juu utakuta mawazo ya biashara telee kisha ingia.