Naombeni ushauri wa kusoma Masters hii ya Open University

Naombeni ushauri wa kusoma Masters hii ya Open University

Joined
Aug 25, 2019
Posts
86
Reaction score
91
Habari za majukumu wanajukwaa, bila shaka ni wazima wa afya.
Naomba niende moja kwa moja kwenye mada yangu;

Ndugu wanajukwaa naombeni ushauri wenu hasa kwa nyie wazoefu na hii kitu inayoitwa "Masters of Arts in International Cooperation and Development" inayotolewa na Chuo kikuu Huria cha Tanzania.

Ndugu wanajukwaa, lengo kuu la kutaka kusoma "Masters" hii ni kuendeleza taaluma yangu pamoja na kutaka kupata maarifa na umahiri zaidi katika hili eneo ukilinganisha na sasa ambapo ninashahada ya Maendeleo ya Jamii. Na ninafanya kazi sehemu kama Afisa Maendeleo ya Jamii.

Ndugu wanajukwaa naomba mwenye uelewa mzuri katika hili eneo anishauri na kunipa mwongozo mzuri.

Ahsanteni sana naomba kuwasilisha mjadala kwenu.
 
Soma gap kwenye taasisi na kazi unayoifanya Mkuu. Kama haviingiliani achana nayo tafuta area nyingine
 
Mkuu ndio maana nikauliza ili mwenye ufahamu mzuri akieleza ndio nitajua kama vinaendana au laa!!
Sasa Mkuu si unasoma description ya kozi husika then unafanya ulinganifu na kazi na kituo cha kazi yako.

Mtu wa kwanza kujua kama inakufaa au laa ni wewe, wa pili ni mwajiri wako (kama ana mipango ya kukutumia), watatu hayupo.
 
Back
Top Bottom