Naombeni ushauri wajasiriamali

Naombeni ushauri wajasiriamali

dlink

Member
Joined
Nov 19, 2011
Posts
69
Reaction score
18
Poleni na kazi,

Mimi ni kijana wa kitanzania, ninashamba la ekari 4 maeneo ya Msata/Chalinze pia nina-mtaji wa Tsh. milioni mbili. Naombeni ushauri nifanye shughuli/biashara gani kupitia rasilimali hizi?
Asante na ntashukuru nikipata ushauri wakunijenga.
 
Tuambie unapenda nini,na hilo shamba ulipewa au ulinunua? Kama ulinunua kwa vyovyote kuna wazo fulani ulikuwa nalo. Toa hilo wazo,tuliboreshe.
 
Asante Kididimo, shamba nililinunua mie mwenyewe, kiukweli nimetafakari sana nini naweza kufanya lakini sijapata jibu zuri ndio nikaona nije jukwaani hapa ni jungu kuu.
 
Mimi niko Mz. Niionavyo Chalinze nikipita kwenda Dar,inakua kwa kasi. Hivyo population inakua kwa kasi. Kuna vihoteli na mama ntilie wengi. Pia kuna watembeza mayai na nyama ya kukuk n.k. Katika mazingira hayo, nenda pale ,fanya utafiti mdogo wa kujua sources yaani vyanzo vya bidhaa zao,bei,na msimu wanaouza sana. Hii inaitwa "market research" yaani utafiti wa soko. Pia unaweza kwenda hadi Mlandizi, na maeneo mengine jirani,hata Dar. Na ili ufaidi eneo lako,na pesa ikue kwa haraka,anza na miradi inayoitwa "quick win projects" yaani inayochukua muda mfupi lakini ina faida.

Utakachokipata katika utafiti wako kama nilivyokueleza hapo juu,anza nacho. Mfano,ingekuwa mimi nimegundua kuwa mazao ya kuku na mbogamboga ndiyo mahitaji makuu,ningeanza na hivyo (gawa eneo mara 2 au 3). Jua ukiwa na miradi miwili tofauti kuna faida! Unapunguza hasara kama kutakuwa na janga (risk) kwa mradi mmoja,na pili miradi itabebana. mfano, ukianza na mchicha au nyanya,utapata fedha ya kuendeleza kuku na kinyume chake. Ziko post nyingi humu kuhusu ufugaji wa kuku na mbogamboga. Pia nashauri kabla ya kuanza kwa kila sekta,mwone mtaalamu wa sekta hiyo aliyekaribu aone shamba,akushauri na uwe karibu naye.
Naamini nimetoa ushauri wa jumla. Utakachamua baada ya utafiti (market research) tupe mrejesho,ninaweza kukushauri vizuri kwenye business plan (Mpango wa biashara)
 
Asante sana Mkuu, umenipa mwanga wakutosha. Wacha nianze na utafiti wa soko, baada ya muda nitarudi kuleta mrejesho.
 
Pale fuga kuku wa mayai na wanyama maana mjini ulaji wa chipsi upo juu pia mbolea ya kuku tumia kulimia mboga mboga nakupa mwaka mmoja tu maisha yako yanabadilika ukisamama vilivyo japo ujasirimali unaitaji moyo na subra.
 
Asante sana Mkuu, umenipa mwanga wakutosha. Wacha nianze na utafiti wa soko, baada ya muda nitarudi kuleta mrejesho.
Nitafurahi kupata mrejesho,na nina hamu ya kuona unafanikiwa kwa kadiri Mungu atakavyojalia.
 
Back
Top Bottom