Naombeni ushauri wakubwa zangu

Acha ujinga wee cindy...long distance relationship ni wizi tuu watu wana nyemka tuu huko. Huyo hakupendi na hapo hamna ndoa.

Alafu wee utakuwa huna tako ndio maana una jisumbua na huyo jamaa.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kuna watu ipo siku malaika watashuka watuchape viboko kwa ujinga wetu.
Yan Mungu kaisha kuonesha kila.dalili kuwa haupo sehemu sahh ila unang'ang'ania tu.
Unayoyaona sasa yategemee kuyaoba na kwenye hio ndoa yenu x100 zaidi ukikubali kuolewa nae
 
Hivi binti wa 23yrs na uko chuo, huu ni muda wa kupambania future ya maisha yako ya baadae, na sio kutegemea mwanaume kupitia mgongo wa ndoa.

Ni heri umeanza kujua mbivu na mbichi bado mapema hivi, ni wajibu wako wee kuchanganua na kuona lipi sahihi kwako jtk maamuzi yako, ndani ya miaka 9 wapo ktk mahusiano ila wana achan na kurudian, hapo ujue huyu mwanaume anakula kwanza ujana akimaliza atavuta mtu ndani kwa ndoa sasa,

Hao wameaanza kusaidian kabla ya kupata kazi, na likitokea tatizo wanakutana na kusolve, pls dea shtuka acha kutumika km daraja ktk mahusiano ya watu, hao watu wanapendan ndo watakao oana, wee unapotezewa muda tyuuh kwa maslahi yao wao.

Kwa kukusihi achana na huyo mwanaume, na usigeuke nyuma ktk hilo, tazama mbele ili kufikia future yako ya maisha yako ya baadae. Km JAH alikupangia ndoa utapata tyuh. Take care.
 
Hebu njoo pm maramoja kuna ujumbe wako wa dharura .
 
Pole sana mdogo wangu; Ushauri wangu
Wewe ni binti mdogo miaka 23, tena inaondekana ni muelewa na unajisomea
Pamoja na kuwa umeongelea zaidi mahusiano yake na huyo mwanamke mwingine; ila nikiangalia kwa undani hamuendani; wewe unaonekana ku forcus kwenye maendeleo wakati mwenzako sio hivyo
Nakushauri uachane na huyo kijana endelea na maisha yako; huyo atakunyima fursa na atakuja kukuacha wakati wale wa kukuoa wamesha oa
Na kwa kuwa upo mkoa wa mbali sana; badili namba na songa mbele.....
 
1.Kimbia upesi sana bila kugeuka nyuma, au kaa kimya milele kama mchepuko mtiifu usimuongelee wala kuulizia chochote kuhusu huyo mwanamke mwingine.
2.Hajazaa kweli na huyo mwanamke? Usikute wana mtoto/watoto kabisa au alishamtolea mahari.Wanaume tuna mengi.
3.Hapo wewe ndo mchepuko, huyo mwanamke mwingine ndo permanent, wewe ndo umeingilia mahusiano ya watu.
 
Ukiendeleza hizo tabia mdogo wangu utajikuta unakubuhu na kuwa mdangaji wa kubeba wanaume za watu. Usichukulie advantage ya wanaogombana kwako ndio iwe ponea yako. Kugombana kupo. Ungekuwa mstaarabu ungewapisha waendelee kugombana hadi watakapopata suluhisho badala ya kuwa mchochezi. Ni mbaya sana hiyo. Utakuja kuaibika.
 
Kisa tu katamka neno "ndoa" basi akili imepata ganzi?
Na ameshakujua shida yako, atakuendesha kwelikweli.

Ushaambiwa hapo juu unaleta usumbufu kwenye mapenzi ya watu, dada hautakiwi.
 
Mahusiano ya mbali ni sawa na kuuziwa kiwanja cha shule ujenge,plz plz achana na uhusiano huo vinginevyo utakuja kujutia maisha yako na muda ambao utapoteza
 
Wanawake ni wabinafsi sana sijawah kuona unatak mwenzako aache stareh alaf ili akuhudumie wew akupe el za nguo mavazi na chakula nzur upate za kueka insta sio hivy acha mwenzio nae afurahie kazi ya jasho lake swala la kukusaidia wew lipo na options haijandikwa kuwa ni sheria akikuoa ndo lazma ila ss iv ni option
 
Aaaah dada acha kuhangaika na watu waloshindikana at 32 mtu bado direction yake haijulikani?umekosa wanaume wa maana?nyie watoto wa chuo mna shida gani?
Kuna mwenzako naye kaambiwa aache chuo akamhudumie mama mkwe wake ni mgonjwa yaani kwakweli wazazi wakisikia mnayofanya huko shuleni wanaweza wakazimia kama siyo kufa
 
huyo ni kama sponsor tu kwako tatizo mabinti wa chuo mnapenda vitu vya bei ya juu kisa show off ila kumbuka kuwa kila mwanaume mwny mafanikio jua kuna mwanamke nyuma yake na ndo huyo anayepata hata nguvu ya kumposti mtanadaoni sio ww .hvyo basi kaa utulie muombe mungu atakupa mwingine hapo umepigwa
 
Tatizo lako ni zito kweli kweli, usipo ni pm utapata madhara makubwa sana kimwili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…