Naombeni ushauri wandugu


Pole sana mama D, ila nahisi huyo mwanaume anapata hela ya kutosha ila sababu inagawanywa familia mbili tofauti na ndio maana inaonekana haitoshi.
Mwambie dadako asitishe misaada kwenye familia ya huyo mwanaume na ajijenge kimaisha vizuri, pia ahakikishe watoto wake wanasoma vizuri bila ya shida.
Haina haja ya kuongea tena na mumewe kuhusu hilo jambo kwani amesalitiwa muda mrefu sana na amejiona ni haki yake kuendelea kumsaliti dadako.
Mwisho aanze maisha kivyake yaani aachane na huyo mwanaume kwani siku hizi magonjwa ni mengi sana.
 
mpe pole mwambie asamehe saba mara sabini
kutenda kosa si kosa,kosa kurudia kosa
 



asante evarm
kweli magonjwa ni mengi.....anaweza kumsamehe sawa lakini magonjwa je??
 
mpe pole mwambie asamehe saba mara sabini
kutenda kosa si kosa,kosa kurudia kosa
kwa hiyo wewe mheshimiwa chapaaa mpenzi wako akizini mara mia mbili natisini na moja ndio utachukua HATUA??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…