- fungua biashara ambayo haitakuhitaji udaiwe kodi, leseni, ushuru na vibali vyovyote kutoka mamlaka husika ili uweze kukuza mtaji wako na hatimaye baadae ndo ufungue biashara yenye anuani na vibali rasmi.
Mf: Banda la chips, kibanda cha matunda, kiosk
- Kama utakuwa na uhitaji wa kuwa na mtu wa kukusimamia biashara yako, epuka kuweka ndugu na marafiki na jitahidi uwe na muda mwingi kufuatilia biashara yako hasa katika kipindi hiki ambacho unaanza
- Epuka kuwajulisha au kuomba ushauri kwa watu wa karibu wanaokujua kuhusu hili unalotaka kulifanya. Tumia mitandao kama hii ambapo ni vigumu kujuana.
- Wazo la biashara litokane na unayopenda kuyafanya, unayoyaweza, unayoyaamini (hata kama hujawahi kuyafanya), yanayowezekana na unayotamani kuyafanya kuliko kuangalia kitu gani kinalipa na wewe ufanye au kuangalia flani anafanya nini na wewe uige ufanye.
- Kila la kheri, mtaji ulionao unatosha sana kuanza safari yako ya kujiajiri. Tegemea changamoto na vikwazo lakini visikurudishe nyuma.