Naombeni ushauri wenu wadau .........

Naombeni ushauri wenu wadau .........

OgwaluMapesa

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2008
Posts
10,942
Reaction score
434
Nina miliki kuwanja maeneo ya kigamboni nilinunua mwaka jana sh milioni 6 ....

Kiwanja kimepimwa na kina hati ya serikali yaani ni kiwanja chenye sifa zote...

Sasa kuna mtu kajitokeza anakitaka kwa sh milioni 12 ....

Pia nilienda benk kuomba mkopo wa milioni 7 wakanikubalia kwa kuwapa hati ya kiwanja ....

Sasa narudi kwenu ... Nikiuze au nichukue mkopo niendeleze biashara yangu ???
 
Biashara gani unataka kuifanya?, kama biashara itakuwa nzuri na endelevu nakushauri uchukuwe mkopo, ardhi ni rasilimali ya kuheshimiwa sana.
 
Nahtaji nifungue stationary na kukuza mtaji Wa mpesa na tgo pesa
 
Usiuze kiwanja chako..miaka mitano ijayo utauza kwa mil.30
 
Kuuza siyo mbaya. Ukipata kiwanja kingine kwa bei nzuri nunua. Hiko uza. Mambo za kukopa si nzuri unakuwa unawafanyia kaz bank bila kujua.

Kuuza nyumba au kiwanja ni kawaida. Si wengine tunauza kila siku na kununua.

Angalizo kama ndio una kiwanja kimoja tu jifikirie mara 2,2
 
Back
Top Bottom