Naombeni ushauri

Naombeni ushauri

Bhokem

Member
Joined
Aug 7, 2009
Posts
37
Reaction score
9
mwenzenu yamenikuta, ninaye BF wangu ambaye 2mekuwa pamoja kwa muda wa takribani miaka 6. Tulipendana sana ktk hiyo miaka sita, hivi karibuni baada ya wote kuanza kazi naona mwenzangu tabia zake sizielewi elewi. Hapendi nitoe hela kuwasaidia ndugu zangu, ingawa mara nyingi anapokuwa safarini hunipigia simu kuwa nimpe ndugu yake fulani pesa na atanirudishia. Sasa wasiwasi wngu ni kuwa tutakapoishi pamoja kama mke na mume, si nitashindwa kabisa kuwasaidia ndugu zangu?:frusty:
 
kwa hiyo hamuishi wote lakini mipango yenu ya fedha huwa mnajadili pamoja au???kwamba unajua ametuaje pesa zake na wewe umetumiaje???
 
kwa wanaume wa kibongo,relationship ya miaka 6 ni mingi mno,itafikia stage mtachokana tu,labda muwe na msimamo wa hali ya juu.kama unamuona mwenzako amebadilika,mueleze,kwani miaka 6 utakuwa tayari,unamjua mtu wako vilivyo.na kama akikuoa,utakachowasaidia ndugu zako,sio lazima umwambie
 
Mwanamke una maamuzi na hela yako kama ilivyo kwa mwanaume.

Unaifanyia kazi,una uhuru wa kuamua matumizi,muelimishe kuhusu hilo mapema,isije kuwa ishu kubwa kwa ndoa.
 
kwa wanaume wa kibongo,relationship ya miaka 6 ni mingi mno,itafikia stage mtachokana tu,labda muwe na msimamo wa hali ya juu.kama unamuona mwenzako amebadilika,mueleze,kwani miaka 6 utakuwa tayari,unamjua mtu wako vilivyo.na kama akikuoa,utakachowasaidia ndugu zako,sio lazima umwambie

Kisukari,huo sasa ndo utakuwa mwanzo wa matatizo,yatakuwa ndo yale yale ya mke kujenga nyumba Sinza akapangisha kimya kimya huku familia inaishi uwanja wa fisi nyumba ya kupanga,siku mume akigundua si patachimbika?
 
pole sana sister,ukiwa na amani nae kubali kuishi naye kama mme ila kama huna amani ondoka mapema
 
Huyo hapendi ndugu atakusumbua tu, napo kama unahisi unampenda sana na hutaki kumpoteza, basi vitu vingine mfiche usimshirikishe kama kuwasaidia ndugu zako, wasaidie kisiri ili uendelee ku mkeep.
 
Back
Top Bottom