Emma El chapo
Member
- Jul 30, 2017
- 30
- 24
Mimi ni kijana wa miaka 28 ninaishi dar, ninaishi na mwanamke huu mwezi wa nne sasa, kiukweli nilikosea kuanzisha mahusiano bila kuchukua tahadhari za kiafya, nikafanya nae ngono zembe kwa muda wote huo, juzi jumatano nikaja kugundua kuwa mwenzangu ni mwathirika wa ukimwi na anatumia ARV kwa usiri mkubwa sana.
Kiukweli nilistuka sana na nilipomuuliza alikubali kuwa mgonjwa na ana mwaka mmoja sasa tangu aanze kutumia dawa, kwa kweli nilichanganyikiwa sana lakini nilipoenda kupima nikajikuta mzima kwa vipimo vya awali na kuambiwa nirudi baada ya miezi 3
Kinachonitatiza nampenda sana yule mwanamke na amekuwa loyal sana kwangu, na mimi ndo msaada wake yeye na familia yake, kumwacha nashindwa kabisa, kila siku anashinda analia anaomba nisimuache mpaka sasa nipo nae home sijui hata nifanyeje naombeni ushauri.
Sent using Jamii Forums mobile app