Naombeni ushauri

ashomile

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2017
Posts
2,739
Reaction score
2,697
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza wakuu,

Mie ni kijana mwenye ndoto umri ( 24 ) na mwenye kipaji upande wa (IT) lakini changamoto yangu ni vifaa vya kazi tu,nakumbuka kabla sijapata kazi niliomba nipate kazi ili ninunue vifaa vya kazi ,lakini leo hii baada ya kupata kazi naona bora nijenge nyumba kwanza na kama ni vifaa ntanunua kwa baadae , isitoshe hii ajira niliyonayo ni kwa muda haijulikani itaisha lini !!

Ila muda wowote Mguu ndani Mwingine nje , kinachoniumiza zaidi nikuona vijana wenzangu wamejenga majumba wakati mimi sina hata bati moja , ila pia nachoona laiti ningepata vifaa vya kazi basi kwa siku kuanzia elfu 20 na kupanda basi ningeifikia kabisa ila sasa nashindwa kutambua nianze na kipi!!

NAWAOMBENI WENYE MAWAZO MNISAIDIE MAANA MPAKA SASA NIKO NJIA PANDA ILA NACHOSHUKURU PESA YANGU BADO SIJAIELEKEZEA KOKOTE .

KARIBUNI SANA MNIOKOE KIJANA MWENZENU .
 
Fanya buzness, I mean (kwa maoni yangu) kama hivyo vifaa vitakua na tija ya kiuchumi kwako (assets) nunua uwekeze ktk muda na taaluma yako.

Nyumba ni Liability sometime,

Jenga kwa profits si vinginevyo.

Pia kuna watu wametumia miaka kama 10, 20 kuandika vitabu, kuna maarifa mengi utajua nn chankufanya. I recommended RICH DAD POOR DAD BOOK WRITTEN BY ROBERT KYOSAKY.

N.K

Mim si mjuaji. ni hayo.
 
Kwani sasa hivyo vifaa vya IT vinagarama ya kujenga nyumba?

Ni mshahara mmoja tu unaweza kutosha kununua vifaa vyote vya IT ingekuwa unataka kuanzisha kampuni kweli
 
Naungana na wachangiaji waliotangulia.

Ni vizuri ukazungusha kipato kidogo ulicho nacho, nyumba utajenga tuu.Usiangalie sana wanaokuzunguka, jiwekee mipango yako, mipango inayoendana na kipato chako.

Hivyo vifaa vya IT ni vifaa gani kwani?
 
Save kiasi fulani ili uanzishe kwanza mradi utakaoweza kuusimamia.
Una taaluma ya kutengeneza mobile apps?
 
Shukrani kwa ushauri
 
Naungana na wachangiaji waliotangulia.

Ni vizuri ukazungusha kipato kidogo ulicho nacho, nyumba utajenga tuu.Usiangalie sana wanaokuzunguka, jiwekee mipango yako, mipango inayoendana na kipato chako.

Hivyo vifaa vya IT ni vifaa gani kwani?
vitendea kazi ndugu yangu .
Computer 1
Laptop 1
Box 3 n.k software
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…