Heshima kwenu wana jamvi.
Nina mpenzi wangu ambaye kweli tuna pendana sana na kwa kweli ni msichana anayeniheshimu na kujiheshimu kuliko wasichana wote niliowajua, lakini kuna sababu ambazo kwa sasa sijaamua kuziweka wazi jamvini zinazopelekea nifikirie kuachana nae.
Lakini ukiachilia hizo sababu ambazo sijaona ni busara kuzimwaga jamvini ni kwamba tunafanya kazi mikoa tofauti, mimi niko dsm na yeye yupo mbeya, na wote tumemaliza chuo kikuu mzumbe, yeye mwaka jana, mimi mwaka juzi.
Sasa wakati nafikiria kuachana naye, huku dsm nako kuna msichana ambaye ni rafiki yangu wa kawaida tu, na ana mazoea nami hadi kufikia kuniita sweet, honey, love etc, ingawa ukweli ni kwamba hatuna uhusiano wowote na hata hivyo aliniambia ana mtu wake na anampenda sana, na mimi pia nilishamwambia kuwa nina mtu wangu, japo tuko mbali.
Sasa jana huyu msichana wa hapa dsm, kaniambia kwamba boyfriend yake sio mwaminifu, na kaamua kuachana nae japo anaumia coz anampenda sana so ameamua kunishirikisha ili nimshauri.
Kwa kweli wana jamvi nipo njia panda, kwa sababu na mimi nimejikuta natamani kum approach huyu dem aliyeachwa na jamaa yake kwa sababu dem wangu kwanza siko naye, so naweza kaa hata zaidi ya miezi miwili nikiwa naugulia hamu ya kufanya mapenzi, na hapa dsm niko more than lonely, nishaurini wakuu, nimtokee huyu dem aliyezinguliwa na mtu wake, then niachane na dem wangu wa kitambo as wanasema fimbo ya mbali haiuwi nyoka, niachane nae kwa style gani, coz naogopa kuumiza moyo wa mwenzangu, isitoshe she is so innocent and decent?
Wakatabahu.
Tt