Ramadhani Juma
Member
- Oct 31, 2011
- 51
- 14
Heshima mbele wakuu. Nipo kwenye lindi la mawazo kwani nimetokea kumpenda mdada mmoja ambaye tunaishi mtaa mmoja. Na nika amua kumueleza hisia zangu kwake akanijibu kwamba tayari nimechelewa. Lakini cha ajabu bado anapenda ukaribu na mimi anapenda kunifahamu, kuwafahamu ndugu zangu na alishawahi kuniambia nimpeleke nyumbani akamuone mama na alipofika alifurahi sana kumuona mama yangu pamoja na ndugu zangu wengi. Je wakuu inaweza ikawa hana mtu isipokuwa ananitega au jamani niachane nae tu maana moyo unauma sana.