Pole kwa yote,
Kwanza nikupongeze kwa kuleta hapa jamvini, naamini utapata ushauri mzuri. Kwanza kabisa kitu cha msingi cha kutambua ni kuwa "HISIA ZA NGONO AU KUHITAJI KUJAMIANA ZINAJENGWA NA MAMBO MENGI", ingawa imekuwa ngumu kwetu wachangiaji kujua kama mna-face circumstance gani hapo kwenu kwani inaweza kuwa mojawapo ya kigezo. Mfano: Inapotokea mmetoka katika ugomvi halafu punde ukataka mjamiane kwa mwanamke inaweza kuwa ngumu zaidi kuwa na hisia kwa tendo husika, ni tofauti sana na maumbile ya wanaume. Lakini hujatuambia kuhusu mwenzi wako kama hiyo hali iko tangu mmeanza mahusiano au imeanza baada ya kuingia ktk ndoa kwa hiyo miaka miwili.!
Kwahiyo ni muhimu sana kumsoma mwenzi wako kabla ya kushiriki kufanya ngono, kama unadhani mwenzi wako hayuko katika mood nzuri basi ni vizuri kuahirisha zoezi, lakini pia wapo watu (hasa wanawake) ambao hisia zao za ngono ziko mbali sana, lakini zikishapanda zinachukua muda mrefu kushuka (kufika kilele).
Kwahiyo ningekushauri yafuatayo:
Jaribu kufanya mambo ya kumfurahisha ikiwa pamoja na mawasiliano mazuri (maongezi, calls, sms), kumletea zawadi ambayo huwa anapenda; hata kama anapenda ice cream au hata pera nunua mpelekee. Toka naye nenda naye sehemu ambayo unadhani atafurahia (outing), kama anapenda mishkaki nanda naye sehemu ya mbali mkiwa wawili mkale mishkaki. Mwambie kuwa unapenda na mwonyeshe hivyo pia... wanaume kwetu inakuwa ngumu kumwambia mwenzi wako kuwa "unampenda" wanawake wanakerwa sana na hilo. Mletee zawadi ambayo ataipenda zaidi, zungumzieni kuhusu mapenzi mara nyingi, hayo yote yana uwezo wa wa kumjengea hisia zaidi za kushiriki ngono.
Mara nyingine, vitu vidogo sana vikamfanya mwenzi wako kukosa hamu ya kushiriki ngono. Kwa wanawake wako tofauti sana na sisi wanaume. Ngono ni sanaa ya hali ya juu sana, inahitaji sana uelewa. Nadhani kwa hayo machache yanaweza kusaidia.