Naombeni wazo la biashara ya million 5 mkoani iringa

Naombeni wazo la biashara ya million 5 mkoani iringa

Aunt shangazi

New Member
Joined
Mar 20, 2024
Posts
1
Reaction score
2
Habari zenu Wana jamvi?

Matumaini mko poa kabisa. Ndugu zangu naomba mwenye uzoefu na mkoa wa Iringa niko na mtaji wa sh. Mil 5 nataka kufanya biashara lakini Hadi muda huu sijui ni biashara gani na nitafanya katika eneo gani mkoani Iringa.

Naombeni sana mawazo yenu
 
Duka la mahitaji ya nyumbani kwa hapo ulipo unaonaje
 
Habari zenu Wana jamvi? Matumaini mko poa kabisa. Ndugu zangu naomba mwenye uzoefu na mkoa wa Iringa niko na mtaji wa sh. Mil 5 nataka kufanya biashara lakini Hadi muda huu sijui ni biashara gani na nitafanya katika eneo gani mkoani Iringa.
Naombeni sana mawazo yenu
1: We katika nafsi yako huwa unapenda kufanya nini ili biashara yako iwe hicho upendacho.

2: kuna changamoto gani unaziona hapo ili uchukue fursa ya kuzitatua?
 
Wekeza kwenye kuchana mbao na chainsaw au anza na biashara ya mbao
 
Anzisha smart mgahawa hakikisha kila chakula kinatoka ktk hadhi na uguse kila uchumi wa mtu,, ukipata eneo min mboni stendi ya bajaji, stendi kuu maeneo ya mashine 3 zamani, ukilenga mazingira hayo hujutiii mzee wangu!
Ishu nyingine fungua ka duka Kadogo Sana lkn kawe kana dili na pombe kali Aina Zote hrf uwe na jiko kubwa la nyama choma, au mdudu jitahid uwe creative Sana yaan ukimbiliwe.
 
Kama upo mjini tuonane nikupe idea na namna ya kuuza hiyo bidhaa ila utanilipa
 
Uza dagaa wa aina zote iringa mjini nimekaa for 5yrs mboga shida sana au ukifeli kabisa uza nguo japo wanauza wengi.
 
Back
Top Bottom