Naombwa kujuzwa madaktari!

kiparah

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2010
Posts
1,173
Reaction score
117
Kwa mfano umepigwa nusu kaputi unafanyiwa operesheni, eti ikiisha kabla ya operesheni kumalizika hairuhusiwa kupigwa tena nusu kaputi? Kwamba mgonjwa akichomwa tena sindano ya nusu kaputi ndo unamuua?
Naomba tu kujuzwa!
 
Kwa hilo kaka linaweza tokea, lkn kwa kitaalam kuna history taking ili kujua vitu mbalimbali vinavyohusiana na mgonjwa anaetakiwa fanyiwa operation kubwa, na kuna watsalamu ambao ndo wenye kazi ya kum - anathetic mgonjwa kabla ya operation kwa kiwango ambacho kitaendana na muda wa operation....
Kwa uzoefu wangu sijawahi kuona mgonjwa akawa amezinduka wakati wa operation!!!
-- ila kwa kawaida kiasi cha pethdin anachopewa kinaweza kumfanya akamka muda zaidi baada ya operation!!
 
Kwa mfano umepigwa nusu kaputi unafanyiwa operesheni, eti ikiisha kabla ya operesheni kumalizika hairuhusiwa kupigwa tena nusu kaputi? Kwamba mgonjwa akichomwa tena sindano ya nusu kaputi ndo unamuua?
Naomba tu kujuzwa!

Mtu(mgonjwa) awapo katika chumba cha upasuaji hawi mwenyewe, kwa kawaida kutegemeana na aina ya upasuaji, kikosi (timu) husika huwa naye mf. Madaktari(wa upasuaji), muuguzi (nesi), mtu wa usingizi, wasaidizi huusika.

Mojawapo ya kazi ya mtu wa usingizi ni kuhakikisha mgonjwa haamki wakati wa upasuaji, ..wakati fulani(kwa sababu nyingi tu) Upasuaji unaweza kuchukua muda zaidi ya ule uliotegemewa, endapo hili litatokea dawa ya usingizi, maumivu huongezwa hivyo kumfanya mgonjwa awe katika hali nzuri ya matibabu/kipimo.

Pia dawa inapokuwa inapungua mwilini, haimaanishi mgonjwa ataamka na kukaa muda huo huo.Hivyo basi mara chache hali hiyo hutokea (dawa ya usingizi) kupungua lakini huongezwa kulingana na mahitaji.
 
Asanteni sana wakuu, Mungu awabariki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…