Naona kama uzee umeshaanza kunisogelea. Ushauri wenu

Cha Kwanza kinga bega uchanjwe, kisha endelea kupiga nyungu maana kuna mgeni mpya wa kirusi cha UVIKO 19 anaitwa lamda.
Mkuu achana na hiyo korona kwanza, rud ktk mada hapo juu
 
Anza kujiandaa kwa vitu vifuatavyo:

1. Afya yako iwe kipaumbele. Kisukari, presha ni magonjwa ya uzee. Punguza matumizi ya Sukari, mafuta na vilevi. Fanya mazoezi madogo madogo.

2. Akiba itakayokusaidia kipindi cha uzee wako iwe kipaumbele. Kama una miradi iendeleze zaidi. Kama kuna kanyumba bado hujamalizia, fanya namna iishe.

3. Focus na familia yako haswa mkeo na watoto. Achana na starehe za kipuuzi. Michepuko ipotezee. Tamaa ya watoto wadogo, ishinde.

4. Kuwa karibu na Mungu. Zidisha ukaribu wako na muumba wako kwa sababu siku zako za kuishi ni chache kuliko zile ambazo tayari uneshatumia.
 
Pamoja mkuu, ahsante kwa ushauri maridhawa
 
Hujataja vitu viwili vya msingi sana kwenye mada yako;
1. Uchumi wako unasimamia wapi kwa sasa.
2. Umri wako.

Baada ya hapo tutajua ushaanza kuzeeka kweli au matatizo ya kiuchumi yanakupa limitations za nini ufanye na nini usifanye.
 
Hujataja vitu viwili vya msingi sana kwenye mada yako;
1. Uchumi wako unasimamia wapi kwa sasa.
2. Umri wako.

Baada ya hapo tutajua ushaanza kuzeeka kweli au matatizo ya kiuchumi yanakupa limitations za nini ufanye na nini usifanye.
Uchumi wangu wa kati, umri kati ya 65-70yrs nacheza hapo bila ya shaka
 
Uchumi wangu wa kati, umri kati ya 65-70yrs nacheza hapo bila ya shaka
Umri kati ya 65-70yrs, basi kwa umri tu bila kuangalia kigezo cha uchumi upo kundi la wazee.

Muhimu ni kujikinga na maradhi yanayoambukiza hasa uviko19. Wewe ni lazima upate hiyo chanjo, lakini usisahau barakoa na jiepushe na misongamano isiyo ya lazima kiongozi.
 
Ushauri wangu hama nyumbani kwa Dada yako.
Tafuta chumba uishi kwa kujitegemea..
 
Jiandae kuota busha na kupungukiwa na nguvu za kiume
 
Nimekupata mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…