Naona kama Vituo vya mwendo kasi ni vikubwa mno

Lihove2

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2018
Posts
3,545
Reaction score
6,512
Jamani nimetafakari sana,nimeona kama baadhi ya vituo vingine vya mwendo kasi walivijenga vikubwa sana bila sababu yoyote.

Mfano hivi vya katikati,Magomeni hospitali,Jangwani,Manyanya etc.Nadhani kuna maeneo ni kweli kuna abiria wengi lakini maeneo mengine abiria ni wachache sana.

Sikuelewa kwanini waliamua kujenga vituo vyenye ukubwa sawa kila eneo.naona kama wangeokea gharama.Hawakuwakufanya need asesment vizuri
 
Walijua tutakaa muda mrefu vituoni tukisubiri haya mabasi kama tunavyokaa sasa.
 
udart ni project ya vizazi hadi vizazi manake kadri siku zinavyoenda na population inaongezeka ikifiki mwaka 2095 vitakua kama msimbazi mwendokas kariakoo
 
Sijui waliiga wapi ila huu mdadi ni kama umewashinda, malalamiko ni mengi kuliko pongezi.
 
Hiyo ndio nzuri mahitaji yakiongezeka hapatahitajika kuongeza kituo
 
Ukubwa wake ni kuwezesha magari mawili au Matatu kusimamia Kwa pamoja katika kituo kimoja na sio wingi wa watu , wapo sahihi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…